Nafasi Ya Matangazo

August 15, 2013

Kulia ni meneja uhusiano wa Airtel jackson Mmbando akimkabidhi  bw Rashid Hamis (kulia) shilingi milioni moja aliyojishia katika droo ya promoshe ya Airtel yatosha wiki hii. Kati wakishudia toka shoto ni  washindi wengine wa milioni moja bw Hamis Athumani  Esia na Bi Magret Kalenge. Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi kuu ya Airtel dar es salaam



Kulia ni meneja uhusiano wa Airtel jackson Mmbando akimkabidhi  bw, Godbless Kweka (kulia) shilingi milioni moja aliyojishia katika droo ya promoshe ya Airtel yatosha wiki hii. Kati wakishudia toka shoto ni washindi wengine wa milioni moja bw Rashid hamis, Bi Magret Kalengea na bw, Hamis Athumani  Esia. Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi kuu ya Airtel dar es salaam
Kulia ni meneja uhusiano wa Airtel jackson Mmbando akimkabidhi  bi, Magret Kaengea (kulia) shilingi milioni moja aliyojishia katika droo ya promoshe ya Airtel yatosha wiki hii. Kati wakishudia toka shoto ni washindi wengine wa milioni moja bw Hamis Athumani  Esia na Rashid Hamis . Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi kuu ya Airtel dar es salaam



Washindi wa milioni moja wa promosheni ya Airtel Yatosha wakionyesha pesa zao walizopokea kutoka Airtel baada ya kuibuka washindi wa siku wa milioni moja, wakishuhudiwa na meneja uhusisnao wa Airtel Jackson Mmbando (kushoto). Kutoka kulia ni Rashidi Hamis, Magreth Kalengea, Hamis Esia na Godbless Kweka.
**********

Airtel ikiwa katika muendelezo huo wa kutoa zawadi imewazawadia
washindi saba wa wiki hii kiasi cha shilingi milioni saba ambapo wateja 7 kila mmoja aliondoka na kitita chake cha shilingi milioni moja kufuatia droo iliyochezeshwa makao makuu ya airtel siku ya jumatatu wiki hii.

Mmoja wa washindi walioibuka na kitita cha shilingi milioni moja ni  Bw. Rashidi Hamis ambaye ni fundi wa magari aliyeeleza wazi kuwa hakutegemea kabisa kupata kiasi hicho cha fedha katika msimu huu na anamshukuru Mungu kwa Airtel kumchagua kama mmoja wa washindi hao.

“Nawashukuru sana Airtel, kwa pesa hii nitaitumia kwa ajili ya shughuli zangu binafsi za kimaendeleo na nategemea itaniendeleza kiuchumi kwa kuweza kuimarisha maisha yangu,” alisema.

Washindi wengine wa milioni moja ni pamoja na John Joseph kutoka Karatu, Gideon Rwegosora kutoka Tanga, Omari Abeid kutoka Shinyanga, Hamis Esia kutoka Dar es salaam, Godbless Kweka kutoka Mtwara na Magreth Kalengea kutoka Dar es salaam.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Airtel Bw. Jackson Mmbando alisema leo tunayofuraha kupata washindi wa promosheni ya Airtel yatosha na kuwakabithi zawadi zao. Washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini  na kujishindia kila mmoja shilingi milioni  moja pesa taslimu kwa kutumia huduma za Airtel yatosha na kujiunga na  vifurushi vyetu mbalimbali.

Wateja wa Airtel wanaweza kujishindia milioni moja kila siku kwa
kupiga *149*99#, chagua 2, chagua kifurushi chochote cha siku, wiki au mwezi kitakacho kufaa. Kumbuka vifurushi hivi pia vitakuingiza moja kwa moja kwenye droo ya Airtel Yatosha Mpaka sasa Airtel imetoa shilingi milioni 37 kwa washindi 37 na inaendelea na promosheni hiyo ambayo inadumu kwa siku 90.

Sambamba na hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni jijini Dar es Salaam bado zinashindaniwa kupitia promosheni ya Airtel yatosha baada ya moja kuchukuliwa na mshindi wa kwanza Bw. Silvanus Juma mkazi wa Iringa.

Posted by MROKI On Thursday, August 15, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo