Meneja wa Airtel mikoa ya kusini
Beda Kinunda (kulia) akimkabidhi funguo ya nyumba mshindi wa nyumba
ya kwanza ya Airtel Yatosha mkazi wa Frelimo mjini Iringa, Sylivanus
Wanga wanaoshuhudia wakati wa makabidhiano hayo jana mjini Iringa
ni mke wa mshindi, Veronica Wanga na Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson
Mmbando .
MSHINDI
wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha, yenye thamani ya Sh milioni 65, amekabidhiwa
rasmi funguo yake mwishoni mwa wiki hii.
Nyumba
hiyo imekabidhiwa kwa mshindi huyo, Silvanus Juma, na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, baada ya kuibuka mshindi kupitia promosheni
maalumu ya Airtel yatosha, shinda nyumba tatu.
Alikabidhiwa funguo zake mkoani Iringa pamoja na cheti kinachoonesha kwamba yeye ni mshindi wa kwanza wa nyumba katika nyumba tatu zinazoshindaniwa kupitia promosheni hiyo.
Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, akizungumza katika makabidhiano hayo,
alisema; “makabidhiano ya funguo hizi ni ya awali, lakini Alhamisi ya wiki
hii Juma atakabidhiwa rasmi nyumba yake
iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.”
Alisema Airtel inayo furaha kumkabidhi mshindi wao huyo zawadi hiyo, na itaendelea kutoa zawadi zilizo bora kwa wateja wake nchi nzima, kupitia promosheni mbalimbali zinazoendeshwa na kampuni hiyo.
“Kama alivyo na furaha mshindi wetu, ndivyo na sisi tunavyofurahi na hii sio kikomo, bado kuna zawadi mbalimbali kwa wateja wa Airtel nchi nzima na cha muhimu ni wao kujiunga na vifurushi mbalimbali vinavyopatikana kwenye promosheni hii ya Airtel Yatosha Shinda Nyumba Tatu ili kushinda,” alisema Mmbando.
Mmbando alisema ili mteja wa Airtel ajiunge na vifurushi hivyo, anapaswa kupiga *149*99# na kuchagua 1 au 2, kisha ajiunge na kifurushi chochote cha wiki, siku au mwenzi.
Mpaka sasa Airtel imeshatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake nchi nzima, ikiwemo Sh milioni 37 kwa washindi 37 na inaendelea na promosheni hiyo ya siku 90. Sambamba na hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni, bado zinashindaniwa kupitia promosheni hiyo.
Akielezea
furaha yake, Juma alisema zawadi hiyo ya nyumba ni bahati ya kipekee ambayo hakuitarajia
hapo awali, na hata alipopigiwa simu hakuamini kwa sababu alijua kitu kama
hicho hakiwezekani, na hawezi kupata nyumba katika msimu kama huo.
“Nilipopigiwa kwanza nilijua ni utani, pengine mtu amejisikia tu kunitania lakini nilipigiwa tena na hapo ndipo nilipoanza kuamini.
Nawashukuru
sana Airtel kwa zawadi hii na ni kielelezo cha wazi kuwa Airtel ni mtandao
unaojali na kuthamini wateja wake,” alisema Juma.
Juma alipatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza katika Makao Makuu ya Airtel Dar es Salaam, mwisho wa mwenzi wa saba mwaka huu.
Viongozi wa Airtel wakiongea na familia ya mshindi hyo nyumbani kwake Frelimo Iringa.
0 comments:
Post a Comment