Mkurugenzi wa Tan Communication
Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis (kulia) akimkabidhi Pikipiki Mfanyakazi Bora wa Kituo hicho Semiyo Sonyo.
**********
Mkurugenzi wa Tan Communication
Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis Amewataka watangazaji na wanahabari wanaofanya kazi katika vituo vya Radio na Televisheni hapa nchini
kuzingatia weledi wa kitaaluma wanapofanya shughuli zao za kila siku ili
kusaidia jamii ya kitanzania kukabiliana na changamoto katika kipindi hiki ambacho
dunia inabebwa na utandawazi.
Akikabidhi pikipiki kwa
mtangazaji bora wa kipindi cha usiku cha LOVE CUTTS kinacho rushwa Radio 5
katika Hafla fupi iliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Robert amesema vyombo vya
habari vya kielectonic yaani Televisheni,Radio, na mitandao ya kijamii
vinafikia watu kwa haraka zaidi na kwa unafuu wa gharama kuliko machapisho na
kwamba vikitumika bila miiko ,weledi na kuzingatia kanuni za kitaaluma vinaweza kuwa
sehemu ya tatizo badala ya kuwa vyombo vya kusukuma kasi ya maendeleo.
Katika tafrija hiyo
Mtangazaji Semio Sonyo amekabidhiwa pikipiki ikiwa ni sehemu ya motisha zinazo
tolewa na kituo cha Radio five kwa wafanyakazi
wake waofanya vizuri
katika majukumu yao.
Semio Sonyo akijaribu pikipiki
aliyokabidhiwa na mkurugenzi wa Tan Communication Media,bwana Robert
Francis
0 comments:
Post a Comment