Na Father Kidevu Blog
MAZISHI ya Mwanafunzi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi AIESEC- IFM, Wende Lwendo wa Mwaka wa
Kwanza Uhandisi Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefariki juzi
kwa kufa maji baharini yanafanyika kesho.
Wende , alifariki katika ufukwe wa bahari ya Hindi
eneo la Kipepeo Kigamboni jijini Dar es Salaam akiogelea na wenzake watatu majira
ya jioni baada ya kumaliza mitihani yao ya kufunga mwaka wa masomo.
Kaka wa marehemu, Sammy Lwendo ameiambia Father
Kidevu Blog leo kuwa marehemu anataraji kuzikwa kesho alasiri katika makaburi ya
Kinondoni na mipango yote ya mazishi inaendelea vizuri.
Lwendo amesema kuwa mipango ya mazishi ilikuwa
ikisubiri wazazi wa marehu ambao waliwasili juzi usiku wakitoakea mkoani Arusha
na kutaarifu ndugu kuwa mazishi yatafanyika Dar es Salaam.
"Marehemu Wende, anataraji kuzikwa Makaburi ya
Kinondoni kesho lakini kabla ya mazishi kutakuwa na ibada itakayofanyika
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni,
"alisema Lwendo.
Lwendo amesema ibada hiyo itaanza majira ya saa 8:00
mchana ambapo pia ndugu jamaa na marafiki watapata wasaa wa kutoa heshima za
mwisho kwa marehemu Wende.
Mmmoja
wa wanafunzi wa IFM, Ester Boswell, ambaye walikuwa wakishi chumba kimoja na
marehremu huko Kigamboni ameelezea msiba huo kuwa ni pigo chuoni kwao na kwake
kwani Marehemu alikuwa ni rafiki yake mkubwa si chuoni lakini hata kabla hawaja
jiunga na chuo hicho.
Boswell
amesema kuwa Marehemu alikuwa ni Rais wa taaasisi ya Wanafunzi wa IFM
ijulikanayo kama AIESEC na alikuwa mhim,ili mkubwa wa taasisi hiyo.
Aidha
amesema kuwa hadi sasa binafsi haamini kifo cha Wendi, huku akielezea kuwa
Marehemu alikuwa ni mtu mcheshi na kuogelea ilikuwa ni moja ya vitu vikubwa
anavyo vipenda.
"Marehemu
alikuwa mpenzi kumbwa sana wa kuogelea na siku zote alikuwa anapenda kwqenda
kuogelea na hata anapokuwa mpweke hosteli huamua kwenda Beach kuogelea na siku
ya tukio aliniaga kuwa anaenda kuogelea na wanafunzi wengine wakiwapo wazungu
ambao wapo katika kubadilishana uzoefu wa kimasomo," alisema Boswell.
0 comments:
Post a Comment