Nafasi Ya Matangazo

July 10, 2013



Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam, wakiangalia ajali ya gari iliyoyahusisha magari mawili, Landrover ya kuvuta magari mabovu T959BAU ambalo iligongwa na lori la mizigo T301AHB lililokuwa na tela T206AGV na kusababisha kifo cha tandiboi wa Land rover, aliyetambulika kwa jina la Abdallah Komba (28) mkazi wa Temeke Mikoroshini.

 Ajali hiyo ilitokea jana barabara ya Mandela. Kwa Mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa Marehemu akiwa na wenzake aliona namna lori lilivyokuwa linakuja kuwagonga wakati wakivuta gari lingine bovu na kuwaambia wenzake wakimbie hivyo nayeye kuruka kushoto na wenzake wakiruka upande mwingine lakini kabla hajamaliza kuruka mtaro lori hilo lilimkanyaga na kumbana na umauti kumfika.
Posted by MROKI On Wednesday, July 10, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo