Shirika la Utangazaji la Sauti ya Amerika Idhaa ya Kiswahili
(VOA) ikishirikiana na USAID limeandaa mkutano mkubwa wa Vijana utakao fanyika kesho mjini Dodoma maarufu
kama Je Nifanyeje?.
Washiriki wa mkutano huo ni vijana mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na Vijana wengine wa mtaani Dodoma wamealikwa kuhudhuria.
Mtangazaji Mashuhuri aliyejiunga na idhaa hiyo mwaka 2008 akitokea kituocha ITV na Redio One Sanday Shomari ndiye atakuwa akiongoza mkutano huo.
Mtangazaji Mashuhuri aliyejiunga na idhaa hiyo mwaka 2008 akitokea kituocha ITV na Redio One Sanday Shomari ndiye atakuwa akiongoza mkutano huo.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari
wa Bunge mjini Dodoma, Sande Shomari pamoja na Bi. Rose Mwakitwange (pichani
juu) wamesema maandalizi ya mkutano huo
yamekamilika na mjadala wake utarushwa moja kwa moja na redio Mshirika ABM FM
ya mjini Dodoma.
Aidha Bi Rose Mwakitwange ambaye aliwahi kuwa C.E.O wa New Habari Group amewataka wanahabari nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuandishi na wazitumie katika kuelimisha umma na kujipatia kipato zaidi.
Mwakitwange amesema kuwa Wanahabari wana wajibu wa kuisaidia jamii kufahamu vitu vingi vinavyowatatizo hivyo Mwandishi wa Habari akitumia vyema taaluma yake ndiye mtu pekee anaeweza kujibu maswali hayo ya jamii katika nyanja mbalimbali kwa kuandika vitu kwa undani na umakini.
Pia amewataka waanahabari kujitokeza na kujiandikisha ili washiriki Mkutano wa Mafuta na Gesi maana utawawezesha kufahamu masuala mbalimbali na kuwapa mbinu za namna ya kuandika habari zihusuzo gesi na mafuta nchini.
0 comments:
Post a Comment