Nafasi Ya Matangazo

June 16, 2013

 Beki wa kati wa Taifa Stars, Kelvin Yondan akijaribu kumdhibiti Kalow Salomon wa Ivory Coast huku mlinda mlango Juma Kaseja akiruka kukamata mpira miguuni kwa Kalow na Eraston Nyoni na Frank Domayo wa Tanzania wakisogea kuongeza nguvu wakati timu hizo mbili zilipokutana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia Brazil 2014 nchini Brazil. Ivory Coast ilishinda 4-2.

 Kikosi cha kwanza cha Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho kilishuka dimbani dhidi ya Ivory Coast Jana.  Mstari wa nyuma walio simama kutoa kushoto ni Mbwana Samata, Erasto Nyoni, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, Kevin yondani na Nahodha Juma Kaseja. Mbele kutoka kushoto-Nadir Haroub 'canavaro', Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Salum Abubakar na Shomari Kapombe.

Kikosi cha kwanza cha Ivory Coast walio simam kutoka kushoto ni, Kalow Salomon, Serey Geoffroy, Bamba Souleman, Traore Lacia, Yaya Toure na Gosso Gosso Jean -Jacques. Msari wa mbele kushoto-Yao Gervals, Aurier Alain,  Nahodha Zokara Didier, Barry Boubacar na Boka Arthur.
 Mbwana Samatta akiwatoka washambuliaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coasta waliokuwa wamezengea lango la Timu ya Taifa Taifa Stars.


Aliyekuwa Kocha wa wekundu wa Msimbazi Simba, Mfaransa Patrick Liewigakipita jukwaani mbele ya wafanyakazi wa NSSF. Mfaransa huyu amerithiwa mikoba yake na Kocha Mzawa Abdalh King Kibaden Mputa aliyewahi kuichezea timu hiyo na kuinoa kwa mara kadhaa.
 Timu za Simba na Yanga ambao ni timu kubwa na zilizo na upinzani mkali leo zilionesha uzalendo wao kwa kuunganisha mabango yao na kuishangilia timu ya Taifa.
 Mdau wa father Kidevu Blog, John Mapinduzi nae alikuwepo uwanjani.
 Hapa ilikuwa ni Msuli tu baina ya Shomary Kapombe (20 mgongoni ) na Aurier Alain.
 Mwamuzi wa mchezo wa leo kati ya taifa Stars ya Tanzania na Ivory Coast Mehdi Abid kutoka Algeria akimwamuru Mchezaji Yaya Toure wa Ivory Cost kuacha kulia lia bali aende akacheze mpira.
 Shomary Kapombe akilia kwa maumivu baada ya kuumua mguu.
 Wachezaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta (10) na Thomas Ulimwengu (11) wakiwa katika heka heka za kutafuta mpira.
Ubao wa Matokeo ulisomeka hivi ..
  
Ras Inocent Nganywagwa nae alikuwepo uwanjani hapo kushuhudia mchezo huo na alipoa badaa ya kutulizwa na Ivory Coast.
 Hakika ni huzuni kwa kila aliye ipenda Taifa Stars...
LICHA ya kufungwa goli 4-2 na Ivory Coast hii leo katika uwanja wake wa nyumbani Timu ya Taifa ya Tanzania imeonesha kandanda safi na lakuvutia ambalo lilikuwa likiwatoa jasho wakali hao wa soka bara afrika.

Ivory Coast ikishusha dimbani wachezaji wake wote wakali wanaosakata soka la kulipwa Ulaya wakiongozwa na Yaya Toure walishikwa na butwaa pale Amri Kiemba alipo pachika bao la kwanza katika dakika ya kwanza ya mchezo huo ulioujazwa watu uwanja wa taifa jijini Dar esa Salaam.

Ingawaje Tanzania inakosa nafasi ya kufuzi fainali za kombe la Dunia 2014 huko Brazil lakini kikosi hicho kinacho nolewa na Kim Poulsen kinaonesha sasa kuiva na kuimarika hivyo kuleta matumaini makubwa zaidi kwa watanzania katika michuano ya AFCON.

Ushindi wa leo wa Ivory Coast inaifanya timu hiyo namba moja Bara Afrika kufikisha pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika kundi hilo na sasa itasubiri kucheza na mmoja wa washindi wengine wa makundi mengine tisa ili kuwania kwenda Brazil mwakani.

Tanzania inabaki na pointi zake sita, huu ukiwa mchezo wa kwanza kufungwa nyumbani katika kampeni hizi na Morocco bila kuhusisha matokeo yake na Gambia, ina pointi tano ikishika mkia wa kundi.  

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mehdi Abid aliyesaidiwa na Hamza Hammou, Bauabdallah Omar wote kutoka Algeria, hadi mapumziko Ivory Coast tayari walikuwa mbele kwa mabao 3-2.

Stars ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao na kuzitumia vyema nyasi za |uwanja wa taifa na kugeuza machinjio ya Tembo wa Teranga mfungaji akiwa ni Amri Kiemba dakika ya kwanza tu aliyepokea pasi ya Mbwana Samatta kufuatia mpira wa kurushwa na Erasto Edward Nyoni kusababisha kizazaa cha piga ni kupige langoni mwa Ivory Coast.

Ivory Coast walishtuka na kujitambua kuwa wapo katika eneo hatari na  dakika ya 15 kupitia kwa Lacina Traore ilisawazisha goli hilo baada ya mabeki wa Stars kuzembea kuokoa huku Mkali wa Man City, Yaya Toure akafunga la pili kwa mpira wa adhabu dakika ya 23, nje kidogo ya eneo la hatari.

Bao hilo lilitokana na wachezaji wa Stars kupanga ukuta wao vibaya na kumpoteza maboya kipa wao, Juma Kaseja aliyeruka bila matumaini kuufuata mpira huo.

Stars walinoa tena kisu chao na kukaza kamba zao vyema kisha kumuweka sawa Tembo wa Teranga na kufanikiwa kupachika bao la kusawazisha kupitia mchezaji wa Kimataifa anaesakata kabumbu huko Congo DRC katika Klabu tajiri ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu hii ikiwa ni kunako dakika ya  35 baada ya kazi nzuri ya Shomary Kapombe.

Hata hivyo, Ivory Coast wakapata penalti rahisi baada ya Gervinho kujiangusha wakati anakabiliana na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kumpa nafasi Yaya Toure mkuachia mkwaju ambao licha ya Kaseja Kuucheza kwa mguu lakini uliingia wavuni dakika ya 43.

Kipindi cha pili Stars ilikianza vizuri na kushambulia mara nyingi langoni mwa Ivory Coast, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi.

Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mdenmark, Kim Poulsen dakika ya 85 baada ya Shomari Kapombe kuumia na kutoka nje na kumuingiza Hamis Mcha  na kumtoa kiungo Mwinyi Kazimoto na kumuingiza mshambuliaji Vincent Barnabas yaliigharimu Tanzania kwa kufungwa bao la nne na kupotea kabisa mchezoni.

Baada ya kutoka Kazimoto, aliyetekeleza majukumu yake vizuri leo, Ivory Coast wakatawala sehemu ya kiungo na kutengeneza bao la nne lililofungwa na Bonny Wilfred akitokea benchi dakika ya 88.

Pamoja na kufungwa, Stars ilicheza soka safi ya kuvutia na mabao yote yalitokana na makosa – na si kuzidiwa uwezo. 

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe/Khamis Mcha dk 85, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto/Vincent Barnabas dk 87, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba.

Ivory Coast; Boubakar Barry, Arthur Boca, Didier Zakora, Solomon Kalou/Sio Giovanni, Gervais Yao, Jean Jarques Gosso Gosso, Alain Aurier, Lacina Traore/Bonny Wilfred, Yaya Toure, Geoffrey Serey na Suleiman Bamba/Nori Koffi Christian.
Posted by MROKI On Sunday, June 16, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo