Nafasi Ya Matangazo

June 09, 2013

 Redd's Miss Sinza 2013, Prisca Element (katikati) akiwa na Mshindi wa pili Happynes Maira (kulia) na Mshindi wa tatu, Sarahy Paul, wakiwa na furaha mara baada ya kutangazwa washindi katika shindano lao lililokuwa likishikiliwa na Redd's Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigitte Alfred.
 Miss Sinza 2012-2013, Brigitte Alfred (kushoto) akimvisha Taji Redd's Miss Sinza 2013, Prisca Element, baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Meeda Club, Sinza jijini Dar es Salaam. 
 Warembo wa Redd's Miss Sinza, wakicheza shoo ya ufunguzi wa shindano lao.
******    ******
Na Mwandishi Wetu
MREMBO Prisca Element jana usiku alifanikiwa kumvua taji la kwanza Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Sinza katika mchuano mkali uliofanyika ukumbi wa Meeda, uliopo Sinza Mori, Dar es Salaam.
 
Brigitte mbali na kushikilia taji la Redd’s Miss Tanzania ndiye pia aliyekuwa mrembo wa Redd’s Miss Tanzania, hivyo kuvuliwa taji hilo la kwanza ni kudhihirisha kinyang’anyiro cha kumsaka mrithi wake kimeshika kasi.
 
Katika shindano hilo lililokuwa kali na la kuvutia, huku burudani ikinogeshwa na kundi la African Stars ‘Twanga Pepeta’, nafasi ya pili ilichukuliwa na Happynes Maira na ile ya tatu akaitwaa Sarah Paul.
 
Warembo wengine wawili waliofanikiwa kuingia katika tano bora walikuwa ni Nicole Michael na Nasra Hassan, ambao walitoa upinzani mkali katika shindano hilo lililokuwa likifuatiliwa kwa karibu na watu wengi.
 
Akizungumza mara baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo, Prisca alisema ana uhakika mkubwa wa kufuata nyayo za Brigitte na kudai atahakikisha anaipigania Sinza kwa nguvu zake zote ili iweze kufanya vyema katika Redd’s Miss Tanzania.
 
Brigitte alipoulizwa kuhusu shindano hilo na kuvuliwa kwake taji, alisema anaamini kwa dhati mrembo aliyechaguliwa atahakikisha kitongoji cha Sinza kinaendelea kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo.
 
“Kikubwa zaidi ni kujiamini na kufuata maelekezo unayopewa, lakini mrembo wetu naamini ana sifa zote zinazostahili na ni matumaini yangu atasonga mbele zaidi katika hatua inayofuata,” alisema.
 
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa inadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) akiwa na Albert Makoye (kushoto) na Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfred, wakishuhudia shindano hilo.
 Shoo ya utangulizi ikiendelea...
 Warembo wakisebeneka na shoo ya ufunguzi.
 Shoo ya ufunguzi, warembo wakiendelea kuwabamba mashabiki wao....
 Mshiriki, Catrina Laurence, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, Nasra Hasan, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, Maua Abdul, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, Doris Mwaipopo, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, Jaqueline Robert, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, ambaye ni mshindi wa pili, Happynes Maira, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, ambaye ni mshindi wa tatu, Sarahy Paul, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, Martha Joseph, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
  Mshiriki, Nicole Michael, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
 Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element na Doris Mwaipopo wakipita jukwaani na vazi la Ufukweni.
 Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza namba 2 Happynes Maira (kulia) na wenzake wakipita jukwaani na vazi la ubunifu.
 Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element, (kulia) na Jaqueline Robert wakipita jukwaani na vazi la usiku.
 Washiriki, wakipita jukwaani na vazi la usiku.
 Warembo wote waliochuana wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutanzwa warembo watano bora.
 Warembo watano Bora, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi, kutoka (kushoto) ni Sarahy Paul, Nasra Hassan, Nicole Michael, Prisca Element na Happynes Maira.
 Mratibu wa shindano hilo Majuto Omary wa pili (kulia) akiwa meza kuu na Mkurugenzi wa Kamatio ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga na wengineo.
 Kalala Junior, akiwaongoza wanenguaji wa Twanga, kushambulia jukwaa wakati wa shindano hilo.
 Warembo watatu wa Miss Ubungo, wakipita jukwaani wakati wakitambulishwa ukumbini hapo, warembo hawa ndiyo wataungana na warembo wa Miss Sinza kuwania Taji la Miss Kinondoni.
 Mkurugenzi wa Usambazi wa Kampuni ya TSN Distribution, Swabir Abdulrehman (katikati) akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu, Sarahy Paul. Kulia ni Meshack Nzowa Ofisa uhusiano wa kinywaji cha Chilly Willy.
 Mratibu wa Masoko na Biashara wa kinywaji cha Dodoma Wine, Frank Matonda, akimkabidhi zawadi mshindi wa pili, Happynes Maira.
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Sinza A, Juma Mgendwa, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza, Redd's Miss sinza 2013, Prisca Element.
Posted by MROKI On Sunday, June 09, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo