Na Mwandishi Wetu,
Arusha
KUTOKANA na mlipuko
wa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu, uchaguzi wa Kata nne jijini Arusha
uliopangwa kufanyika leo umeahirishwa na kupangwa tena kufanyika Juni 30 mwaka
huu.
Uchaguzi huo umeahirishwa
huku mlipuko wa jana ambao ulitokea wakati Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia
na Maeendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anafunga mkutano wake, ulisababisha
kuzuka kwa taharuki kubwa katika mkutano huo wa kampeni.
Watu kadhaa
wamehofiwa kufa katika mlipuko huo, ambao umezidi kuomnyesha kuwa hali ya amani
kataika Taifa hili la Tanzania inazidi kutoweka.
Mwandishi wetu jijini
Arusha, aliiambia Handeni Kwetu kuwa uchaguzi huo umeahirishwa. Bado tunafuatilia
kwa kina mtifuano huo sambamba na hali za majeruhi na waliopoteza maisha.
Mlipuko huo ulitokea
na kuleta wasiwasi mkubwa katika kazi za kijamii, kama vile mikutano na
makongamano pale yanapohusisha watu wengi na kuleta hofu kubwa.
0 comments:
Post a Comment