Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya hisani itakayowakutanisha
waheshimiwa wabunge na Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini Dodoma,
ambapo huko mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo lengo la
mechi hizo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya albino, huku kukipangwa
kuwa na burudani za kila aina, sambamba na wasanii watakaoamua kuungana na
serikali juu ya uchangiaji huo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu
hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo
Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi, ila wamejipanga
imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi wabunge, ambao baadhi yao wameanza
kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake.
Alisema kuwa Watanzania wote watakaopata fursa ya kuhudhuria
kwenye mechi hizo wataaburudika kwa kiasi kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya
wakuu wa wilaya wengi kuwa mikoani, ila wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya
wabunge.
“Tupo imara na tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu kwa
kukutanisha wakuu wa wilaya wote waliokuwa kwenye timu hii, huku barua za
kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa Mikoa tayari zimeshafika kwa ajili ya
kufanikisha zoezi hili.
“Katika mechi hizi, mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald
Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa
ni IGP Said Mwema na Stephen Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo
huu,” alisema.
Aliwataja Wakuu wa wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi
hicho kuwa ni pamoja na Venas Mwamoto (Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman
Sigara (Mbeya), Krispin Meela (Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo
(Chunya), Herman Kapufyi (Same), Francis Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu),
Yahya Nawanda (Iramba), Elibariki Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu),
Paza Mwamlima (Mpanda), Abdallah Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela
(Arusha), Konstantin Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe),
Muhingo Rweyemamu (handeni), Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima (Bariadi), Jordan
Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela Rubinga (Mpanda) nay
eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni msemaji wa timu hiyo.
Aidha, Muhingo alitaja kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa
na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba (Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa
(Pangani), Mboni Mgaza (Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida),
Angelina Mabula (Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha (Urambo)
Jacqueline Liana ( Magu).
0 comments:
Post a Comment