Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kishapu wakichota maji kwenye mto.
Harakati za utafutaji maji.…
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kishapu wakichota maji kwenye mto.
Harakati za utafutaji maji.
Heka heka za utafutaji maji eneo la Mto Tungu.
Mchuuzi wa maji Kijiji cha Mhunze akichota maji kwaajili ya kuuza. Dumu moja huuza wastani wa sh 500.
Mmoja wa waandishi wa habari kutoka Thehabari.com akinywa maji kwenye kisima cha muda.
Shida ya Maji Kata ya Kishapu haipo kwa wananchi pekee hata wanyama. Hapa nao wanapita kunywa maji baada ya malisho.
******
Na Thehabari.com,
Kishapu
WANASEMA
maji ni uhai, kinyume chake bila maji hakuna uhai wa mwanadamu na hata wanyama.
Kimsingi kauli hii inaonesha umuhimu wa maji katika maisha ya kila siku ya
binadamu na hata viumbe wengine.
Shughuli
nyingi zinazofanywa na mwanadamu kila siku zinategemea uwepo wa maji. Matumizi
ya maji kwa shughuli za binadamu hayaepukiki. Na hata katika mwili wa binadau
ni muhimu zaidi, kama huto yaitaji maji kwa kunywa utayahitaji kwa kuoga na
usafi wa shughuli nyingine.
Kwa
mantiki hiyo hali yoyote ya upatikanaji ngumu ya upatikanaji wa maji unaathiri
maisha ya kila siku ya mwanadamu. Shida ya huduma ya maji eneo fulani huweza
kuchangia ugumu wa maisha kiasi fulani. Shida ya maji maeneo mengine huweza
kupunguza shughuli za uzalishaji mali, hii ni kutokana na muda mwingi kupotezwa
na jamii kwa ufuatiliaji wa maji hasa maeneo ya vijijini.
Hali
kama hii ya shida ya huduma ya maji ndiyo inayowakumba wananchi wa vijiji anuai
vya Kata ya Kishapu, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. Kata ya Kishapu ina
vijiji nane yaani Mhunze, Lubaga, Isoso, Mwanuru, Migunga, Mwamagembe, Mtaga,
na Kishapu yenyewe.
Japokuwa
vijiji vingi vina shida kubwa ya huduma za maji, lakini hali ya ugumu wa
upatikanaji huduma hizo hutofautiana kutoka kijiji kimoja hadi kingine. Kati ya
vijiji vyote nane vijiji vinne ndio vyenye shida ya maji zaidi. Vijiji hivyo ni
pamoja na Lubaga, Isoso, Mwanuru na Kishapu yenyewe.
Zifuatazo
ni picha anuai zikionesha wananchi wanavyoangaika kutafuta huduma za maji
vijiji hivyo.
0 comments:
Post a Comment