Makamu
wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally
Iddy akipokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za baraza la
wawakilishi za mpira wa miguu na pete toka kwa Meneja masoko wa kinywaji
cha Grandmalt Fimbo Mohamed Butallah kwenye makabidhiano yaliyofanyika
kwenye ukumbi la baraza la wawakilishi Zanzibar, kushoto kwake ni
mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza Hassan
Juma.
Makamu
wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally
Iddy pichani kati akiwashukuru Grand Malt kwa msaada mkubwa walioutoa wa
vifaa mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),wakati alipokuwa akipokea
vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za baraza la wawakilishi za mpira
wa miguu na pete toka kwa Meneja masoko wa kinywaji cha Grandmalt Fimbo
Mohamed Butallah kwenye makabidhiano yaliyofanyika kwenye ukumbi wa
baraza la wawakilishi Zanzibar. kushoto kwake ni mwenyekiti wa timu ya
Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza Hassan Juma.
Meneja
masoko wa kinywaji cha Grandmalt Fimbo Mohamed Butallah akizungumza
machache kwenye makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa Makamu
wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally
Iddy wakati alipokuwa akipokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za
baraza la wawakilishi za mpira wa miguu na pete yaliyofanyika
kwenye ukumbi la baraza la wawakilishi Zanzibar, kushoto kwake ni
mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza Hassan
Juma.
========== ====== ========
TIMU
za Baraza la Wawakilishi za mchezo wa soka na netiboli, mwishoni mwa
wiki zilikabidhiwa vifaa vya michezo vya aina mbalimbali ili kuziwezesha
kushiriki mashindano mbalimbali kwa uwezo zaidi.
Vifaa
hivyo vilitolewa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, ambao
walisema kutokana na kuamua kuwekeza katika michezo Zanzibar, waliona ni
vema kuvikabidhi pia kwa timu za Baraza la Wawakilishi ili wajumbe wake
waweze kuwa sehemu ya maendeleo ya michezo hapa nchini.
Akikabidhi
vifaa hivyo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Balozi Seif Idd, Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo Butallah
alisema, wataendelea kuwekeza katika miichezo kwani wanaamini itatoa
fursa kubwa kwa watu mbalimbali kushiriki na hata kuongeza kipato kwao.
“Grand
Malt ikiwa ni wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar, iliona vema
ikatoa msaada huu wa vifaa vya michezo kwa timu za Baraza la
Wawakilishi, ili wajumbe wake wawe sehemu ya kuendeleza michezo hapa
nchini,” alisema.
Akipokea
msaada huo, Balozi Seif aliishukuru Grand Malt na kuiomba pia idhamini
sherehe za Mapinduzi Zanzibar na akataka zitayarishwe mbio fupi ambazo
wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi watashiriki, huku akiahidi atakuwa
mmoja wao.
“Grand
Malt ni kinywaji cha afya kwasababu hakina kilevi, naomba waendelee
kutusapoti katika mambo mbalimbali na tukumbuke michezo ni afya, hivyo
pia ingekuwa vema mngeaa mbio fupi kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi,
nami naahidi nitashiriki,” alisema.
Grand Malt kinywaji kisicho na kilevi kwa sasa ndio wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment