Mkurugezi
wa mauzo na masoko wa Airtel bw Mustafa Kapasi (kushoto) akimkabidhi
cheti cha kuhitimu mafunzo Afisa mauzo kanda ya dar es salaam Airtel
John Gondwe baada ya kuhitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji ya muda wa
miaka miwili yanayoendeshwa na Airtel
Centum Sales University (ACSU). Wafanyakazi 56 kutoka katika mikoa
mbalimbali walihitimu mafunzo hayo, akishuhudia katikati ni Mkurugenzi
Rasilimali watu Patrick Foya akifatiwa na Melvin Joel Meneja wa Centum
Learning Makao Makuu.
Meneja Mauzo wa Airtel Bw Stratory Mushi (katikati) akiwa katika picha ya pomoja na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel
Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika
ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa
Airtel Tanzania.
wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel
Centum Sales University (ACSU) wakikata keki kwa pamoja wakati wa
tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco.
Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania
Mkurugenzi wa Airtel Bw Sunil Colaso akiongea na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel
Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika
ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa
Airtel Tanzania.
***** *******
Airtel Tanzania, mtandao wa mawasiliano wenye
gharama nafuu nchini leo imewakabidhi shahada wafanyakazi wake 56
waliohitimu mafunzo ya mauzo ya muda wa miaka miwili yanayoendesha na
Airtel Centum Sales University (ACSU).
chuo cha masoko cha Airtel Centum Sales
University kilizinduliwa Tanzania mwaka 2011, lengo la kuwaanda na
kuwawezesha wafanyakazi wa Mauzo na usambazaji kupata ujuzi bora, elimu
ya mauzo na usambazaji utakaowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi
na kuhakikisha wauzaji wa rejareja wanaongeza ufanisi na kuongeza tija .
Akiongea katika halfa ya mahafali ya wahitimu
hao yaliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Moroco,Mkurugenzi wa
Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso alisema,” Programu hii ya Airtel
Sales Academy inatolewa na Taasisi ya ukufunzi ijulikanayo kama Centum
learning inayotoa mafunzo ya mauzo na usambazaji na kuwawezesha
wafanyakazi wa Airtel kuwa bora zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla.
tunawapongeza wafanyakazi wetu kwa kazi nzuri waliofanya katika kipindi
chote cha mafunzo yao na tunaamini kwamba mafunzo waliyopata ya
masoko na usambazaji yataleta mabadiliko na kuwapa wateja wetu huduma
bora na zenye viwango vya juu ambazo hazijawahi kupatikana Tanzania.
Airtel tunaamini mikakati na malengo
tuliojiwekea haitakuwa na tija bila kuwa na wafanyakazi wenye vipaji,
wenye hari na nguvu watakao tumika kama vyombo muhimu kufanya ndoto na
mipango yetu kuwa ya hakika aliongeza Colaso.
Airtel tunamini wafanyakazi ndio nguzo muhimu
katika kuleta mabadiliko ya kitamaduni , kasi ya kazi na kibiashara.
kampuni imewekeza katika kukuza uwezo wa wafanyakazi na kutoa nafasi ya
kukuza fani zao ndani ya kampuni. Mafunzo ya ujuzi daima imekuwa ni
mikakati yetu inayoendana sambamba na ujuzi unaohitajika kimataifa.
Mafunzo ya ACSU yalianzishwa
India mwaka 2009 yakiwa na lengo la kuongeza ujuzi, maarifa na ufanisi
endelevu kwa wafanyaka wa mauzo. Mpaka sasa zaidi ya wafanyakazi
80,000 wa vitengo mbalimbali wamepata mafunzo hayo.
Taasis ya Centum Learning
inamilikiwa na Bharti na inatoa mafunzo yanayosaidia kuongeza ujuzi na
kuleta ufanisi katika nchi 17 zikiwemo Africa, India, Bangladesh and
Sri-Lanka.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Centum Learning tembelea www.centumlearning.com
0 comments:
Post a Comment