Mwandishi Wetu, Moshi
KATIKA kuelekea mchezo wa jana
dhidi ya Flamingo FC ya Arusha, Machava FC ambo ndio mabingwa wa ligi daraja la
Tatu, mkoa wa Kilimanjaro, wamekabidhiwa vifaa vya michezo na uongozi wa chama
cha Mapinduzi CCM wilaya ya Moshi.
Machava FC walikabidhiwa vifaa
hivyo ambavyo ni mipira mitano na Jezi, kama sehemu ya mchango wa Chama hicho
kwa timu hiyo ambayo kwa sasa ndio inayobeba Roho ya mkoa wa Kilimanjaro katika
medani ya soka.
Akizungumza baada ya kukabidhi
vifa hivyo vilivyotolewa kwa timu hiyo na Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM, Jerry
Silaa, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini Aluu Segamba aliwahakikishia wapenzi
wa soka mkoani hapa kuwa wako tayari kushirikiana nao hadi mwisho wa Safari.
“Leo tunatimiza ahadi yetu kwa
wawakilishi wetu, mabingwa wa Mkoa timu ya Machava, tunaamini kuwa timu hii
kama roho ya kilimanjaro katika mchezo wa soka itafanya makubwa na
kinachotakiwa ni kuwapa sapoti inayostahili,” alisema Segamba.
Naye Makamu Mwenyekiti wa
klabu hiyo Abuu Masoud, baada ya kupokea msaada huo kutoka CCM, alisema
kutokana ushirikiano unaoneshwa na wadau wa soka kwa timu yao wanaahidi kufanya
vizuri katika michezo yao yote na kuwapa raha wapenzi na mashabiki wa Machava
mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande kocha msaidizi wa
machava aliwaondoa hofu mashabiki wa timu yake kuhusu hali ya Afya ya
mshambuliaji wa kutumainiwa wa klabu hiyo, Isa Kipese na kuelekea mchezo wa
jana na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni ripoti za madaktari wanaomshughulikia
mchezaji huyo.
Katika hatu nyingine
chama cha Mapinduzi CCM pia imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya
Gillete Fc ya kata ya Kaloleni kama sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama
hicho za kutoa fursa nyingi za ajira kwa njia ya michezo.
Akikabidhi vifaa hivyo, mipira
miwili na Jezi kwa diwani wa kata ya Kaloleni, Michael Mwita, Segamba alisema
kuwa wanalenga kuunganisha umma wa mkoa wa Kilimanjaro, kupitia michezo na
kuongeza kuwa katika swala la michezo watu wote ni ndugu bila kujali itikadi
zao.
0 comments:
Post a Comment