Katibu wa Kikundi cha Usindikaji Korosho cha Tujiamini akipanga pakiti za Korosho tayari kwa kuwauzia wateja katika Stand kuu ya Mabasi Lindi Mjini.
Mkoa wa Llindi wakazi wake
wengi ni wakulima hasa maeneo ya vijijini wengi wanalima mazao mchanganyiko
yaani ya biashara na chakula mazao ya biashara hasa ni Korosho ambazo
zinapatika kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa,Lindi Vijijini,na Nachingwea.
Pia kuna zao la Ufuta na
ndizi kama zao la biashara na chakula pia Mazao ya chakula kuna
mahindi,mpunga,muhogo,nyanya,vitunguu hizi pia ulimwa sana wakati wa masika
kutegemea na mvua za vuli.
Biashara wakazi wengi wa
mkoa wa Lindi wanafanya biashara hasa biashara ndogondogo zijulikanaza kama
machinga trade wanauza mazao wakati wa mavuno na uchukua bidhaa nyingi kutoka
Dar-es-Salaam na kupeleka vijijini hasa kwenye Kata.
Camera ya Father Kidevu
Blog leo katika pita pita na mulika mulika yake ndani ya Mkoa wa Lindi hasa
Lindi mjini ilibahatika kukutana na akina mama wanao unda kikundi cha
uzalishaji na usindikaji Korosho kijulikanacho kama TUJIAMINI CASHNUTS
PROCESSING FOOD.
Tujiamini, kama lilivyo
jina lake ni kundi la waakina mama ambalo linalenga kuwajengea uwezo akina mama
kuweza kujiamini katika maisha kwa kuwa na kipato chao cha kuendesha maisha yao
na familia pia.
Akizungumza na Father
Kidevu Blog, Katibu wa Kikundi hicho Bi. Salma Mmole amesema wao hununua bidhaa
hiyo kutoka kwa wakulima na kuisindika kulingana viwango vinavyohitajika katika
masok a ndani na nje ya Tanzania.
Ujazo wa paketi zao ni
kuanzia zile za Tsh 2,000/= hadi 15,000/= na zipo Korosho Nyeupe, Za kuokwa na
zakawaida zilizozoeleka maeneo mengi.
“Soko letu kubwa ni kwa
watu wa aina zote hasa wasafiri wa ndani ya mkoa wa Lindi na nje ya Mkoa, bado
hatujawa na masoko ya uhakika hasa katika Mahoteli makubwa na Maofisi lakini
Fursa ya namna hiyo ikitokea Biashara itakuwa zaidi,” alisema Salma.
Aidha alisema kuwa yeyote
atakaependa au kuhitaji Bidhaa hiyo kutoka kwao ili nao waweze jikwamua
kimaisha wawasiliane nao kupitia Simu ya ofisi 0715397110.
Katibu wa Tujiamini Cashnuts akijaza moja ya pakiti za korosho zilizookwa tayari kwa kuwauzia wateja wao katika eneo la Stand Kuu ya Mabasi Lindi.
Baadhi ya wana kikundi cha Tujiamini wakiwa katika eneo lao la biashara stand.
Katibu wa Kikundi akipanga Korosho
Wateja hujitokeza kununua bidhaa hiyo kwa matumizi ya kawaida
Korosho za kawaida zikiwa sokoni...
Pakiti za Korosho Nyeupe
Hii ni pakiti ya Shilingi 15,000/= ya Korosho iliyo Okwa.
0 comments:
Post a Comment