Mnara maalum ambao unautambulisha mkoa wa Lindi.
Camera ya Father Kidevu Blog leo imevinjari na kupata
taswira kadhaa za mji wa Lindi.
Licha ya Mkoia huu kuanzishwa tangu mwaka 1971 ukiwa na
ukubwa wa eneo Kilometa za mraba 67,000 km². Karibu robo ya eneo
lake au 18,000 km² ni sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous.
Mkoa wa Lindi umepakana na mikoa ya Pwani,
Mtwara,
Ruvuma
na Morogoro.
Upande wa mashariki hupakana na Bahari Hindi.
Mkoa una wilaya sita za Lindi Mjini,
Lindi
Vijijini, Kilwa, Nachingwea,
Liwale
na Ruangwa.
Lindi mjini bado inaonekana
kama vile ilivyo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na namna mji huo
ulivyo na kukosa hadhi kabisa ya kuonekana kuwa ni Mkoa, waweza sema kuwa ni
Mkoa ambao umesahaulika kimaendeleo jambo ambalo linawafanya wananchi pia
kujongea taratibu kwa maendeleo maana hadi hivi sasa zipoi nyumba za nyasi na
zilizoezekwa kwa makuti katika baadhi ya mitaa mjini.
Mito mikubwa ndiyo Lukuledi,
Matando na Mavuji, yote yaelekea Bahari Hindi. Mwinuko huanza mwambaoni
ukipanda hadi mita 500, hakuna milima mirefu sana.
Kuna barabara chache katika
hali nzuri. Ndizo 155 km za barabara ya lami na 3567 km barabara za udongo,
mara nyingi katika hali mbaya. Wakati wa mvua mara kwa mara njia ya kwenda Dar es Salaam
imefungwa. Kuna matumaini ya kuboreka kwa mawasiliano na mji mkuu wa Daresalaam
tangu kumalizika kwa daraja la Rufiji.
Kwa sasa barabara ya kutoka
Mingoyo mpaka Dar-es salaam imekamilika kwa kiwango cha lami ni kimebaki
kipande cha kilometa 60 tu kuanzia Muhoro wilaya ya kilwa mpaka kukaribia
daraja la Mkapa mto Rufiji ambacho kinamaliziwa kwa kiwango cha lami.
Pana kiwanja cha ndege
Lindi, Nachingwea na Kilwa Masoko. Lindi na Kilwa Masoko kuna pia
bandari. Huduma za simu zipata maendeleo kiasi tangu kuanzishwa kwa simu za
mkononi.
Utalii haujafikia umuhimu
sana kutokana na matatizo ya mawasiliano magumu ingawa Lindi ina sehemu
mbalimbali zenye uwezo wa kuwavuta watalii: Kilwa
Kisiwani ndicho mji wa kihistoria wa pwani la Afrika ya Mashariki
pamoja na magofu ya miji mingine ya Waswahili,
Selous ni hifadhi kubwa kabisa katika Afrika, ufukoni wa mchanga ni wa kuvutia
sana, nafasi za zamia majini ni tele.
Gesi imepatikana baharini
karibu na kisiwa cha Songosongo imeleta matumaini ya maendeleo.
Jengo la Ghorofa mbili la shule ya Msingi Stadium ilipo jirani na Uwanja wa Michezo wa Ilulu mkoani Lindi.
Mikoa mingi ya Mwambao wa Pwani hukosi wachuuzi wa Madafu mitaani...
Maji hupatikana katika visima vilivyopo katika nyumba nyingi za Mkoa huo.
Hapa ni mjini kabisa lakini miundo mbinu ya barabara bado ni duni...
Kidogo baadhi ya maeneo kuna lami...
Mitaa mingi ni vumbi ...
Hapa ni stendi kuu ya mabasi yanayoenda kila kona ya mji huo wa Lindi
0 comments:
Post a Comment