Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia)
akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya
ushirikishwaji wa raia katika mchakato wa uanzishwaji wa Jumuia ya Afrika
Mashariki (EAC) uliofanyika jan a jijini Dar es Salaam. Pamoja nae ni Mwenyekiti
wa Jukwaa la Dira ya Afrika Mashariki (VEAF),
ambao ndio waliofanya utafiti huo,Dr. Azaveli Lwaitama.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi
(katikati) akizindua kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya ushirikishwaji wa raia
katika mchakato wa uanzishwaji wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC). Pamoja nae
ni Katibu Mkuu wa zamani wa EAC, Balozi Dk. Juma Mwapachu (kulia) na Mwenyekiti
wa Jukwaa la Dira ya Afrika Mashariki (VEAF),
ambao ndio waliofanya utafiti huo,Dr. Azaveli Lwaitama.
Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (walioketi katikati) akiwa pamoja na washiri wa Kongamano hilo. ****** *******
Na Mtuwa Salira wa EANA
Rais wa zamani wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi
amependekeza kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutangaza
Novemba 30 kuwa siku ya mapumziko kwa nchi zote za jumuiya hiyo ili kuongeza
uelewa wa wananchi wake juu ya masuala ya mtangamano.
Novemba
30, 1993 ilikuwa ndiyo siku ambapo Kamisheni ya Utatu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ilizinduliwa na hatimaye kuzaliwa upya kwa jumuiya hiyo iliyokufa
mwaka 1977. Hivi sasa tarehe hiyo inaadhimishwa kama Siku ya EAC lakini siyo
siku ya mapumziko katika nchi wananchama.
Mwinyi
alitoa mapendekezo hayo Jumatano jijini Dar es Salaam alipozindua ripoti ya
utafiti wa kwanza wa Afrika Mashariki juu ya ushiriki wa raia katika
mchakato wa ushirikiano wa EAC, uliyofanywa na Jukwaa la Dira ya Afrika
Mashariki (VEAF) ambayo imebaini kwamba upo ushiki hafifu wa raia katika
mwenendo mzima wa mchakato huo.
''Nitakuwa
na furaha zaidi kutoa mchango wangu wa kuwashawishi marais waliopo sasa ili
kutangaza Novemba 30, 1993, siku ambayo Tume ya Utatu ya Afrika Mashariki
ilipozinduliwa mjini Arusha, marehemu Mwalimu Nyerere akiwepo, kuwa Siku ya
Afrika Mashariki,'' alisema Mwinyi ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania.
Alisema,
siku kama hiyo wananchi pamoja na mambo mengine wanaweza kufanya shughuli
mbalimbali ikiwa ni pamoja na maonyesho ya utamaduni na bidhaa za kilimo na
viwanda katika majiji yote na mipakani, ambapo alisema, mwisho wa siku
vitaongeza uelewa wa wananchi juu ya jumuiya yao ya Afrikia Mashariki.
Sehemu
ya ripoti hiyo ilisema ingawa kuanzsihwa upya kwa jumuiya hiyo kulilenga iwe na
misingi yake kwa wananchi, matokeo ya u
0 comments:
Post a Comment