Picha ya Marehemu Jaji Mstaafu Ernest Mwipopo
Majaji
wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest
Mwipopo, wakishusha katika gari kwa ajili ya kuanza shughuli za kuaga
katika viwanja vya Karimjee, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji
Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3,
huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika
leo April 5, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,
ambapo baada ya shughuli hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa
kwa maziko kesho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwafariji ndugu wa marehemu baada ya kutoa heshima za mwisho, wakati
wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest
Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro.
Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika leo April 5, 2013 kwenye
Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo
mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko kesho.
Mmoja wa wanafamilia akibugujikwa machozi wakati wa shughuli hiyo ya kuaga.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na Jaji Mkuu Kiongozi na Jaji Mkuu wakati akiwasili kwenye
Viwanja vya Karimjee leo kushiriki kwenye shughuli za kuaga mwili wa
marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya
gari April 3, huko maeneo ya Morogoro.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Jaji Mkuu
Kiongozi na Jaji Mkuu wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga mwili.Picha
na OMR
0 comments:
Post a Comment