Afisa
Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa simu
Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha
wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye
technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika
275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu
Monday 15 Aprili 2013, Airtel Tanzania imeungana kwa pamoja na kampuni ya Nokia na kuzindua simu ya Nokia Lumia 620 itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kuunganishwa na huduma ya technologia ya juu kwa kupitia simu za kisasa na kupata ofa kabambe za bure za muda wa mongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet kwa muda wa mienzi mitatu.
Nokia Lumia 620 pamoja na simkadi ya Airtel itatoa uwezo tofauti ikiwemo kuunganishwa na internet na mtandao na kuangalia mitandao mbalimbali yakijamii pamoja na tovuti mbalimbali. Nokia Lumia inamuonekano mzuri na wa kisasa wenye rangi za kipekee ambapo kutokana na ubunifu `wetu wa kutengeneza simu zenye rangi tofauti mteja ataweza kujichagulia simu yenye mvuto na rangi aitakayo Vitu vingine vilivyopo kwenye simu hii ya Nokia Lumia ni pamoja na kamera yenye lensi ya kisasa, ya mega pixel 5, pamoja na kamera ya mbele, kutokana na kuwa na Lensi bora hii itamuwezesha mteja kupata video au picha yenye muonekano mzuri zaidi Ndani ya Nokia Lumia 620 unaweza kupata vitu muhimu sana ikiwemo ramani ya Dunia pamoja na maelekezo maalum wa vitu au sehemu maalum mbalimbali.
Akiongea wakati wa uzinduzi Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” tumeshirikiana na Nokia katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora na nafuu kwa kupitia vifaa vya Nokia vinavyokuhakikishia kiwango cha juu huku tukiwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu”.
“Kwa kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G tunayoitoa nchi nzima wateja wetu wana hakikishiwa huduma za uhakika wakati wote.
Nokia Lumia itaunganishwa na ofa ya kifurushi cha muda wa maongezi cha dakika 275, sms bila kikomo na intenet ya kifurushi cha 3GB kitakachopatika kwa wiki moja kila mwenzi kwa muda wa mienzi mitatu”.
“Kupata offa hii wateja wetu watatakiwa kuweka muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi 1000 mara wanaponunua simu ya Nokia Lumia 620.
Na
katika kuthibitisha thamira yetu ya kutoa huduma zinazoendana nathamani ya pesa ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu.
0 comments:
Post a Comment