Na
Johary Kachwamba na Eleuteri Mangi _MAELEZO
WANACHUO Shule za biashara kutoka vyuo vikuu
nane (8) mbalimbali vya Afrika Mashariki
wanatarajia kukutana ili kujadili fursa za ajira katika nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ilitolewa jana (leo) jijini Dar es
salaam na Rais wa Wanachuo wanasoma masomo ya Biashara (Dar es salaam
University Finance Association -DUFA) Maximillian Msuya wakati wanaongea na waandishi wa habari.
Alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuzungumzia
maswala ya sekta ya mafuta na gesi na vilevile
watazungumzia mitaala ya elimu katika eneo la Afrika mashariki.
Msuya aliongeza kuwa mkutano huo utaangalia namna gani nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaandaa
wataalamu katika soko la ushindani la ajira za kuajiriwa na zile kujiajiri
wenyewe.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi
ya tarehe 16 mwezi huu, katika Chuo Kikuu
cha Dar-es-salaam.
Rais huyo ametaja vyuo vitakavyoshiriki kuwa ni Chuo
Kikuu cha Nairobi (UON), Chuo Kikuu cha Kisii na United States International
University (USIU) kutoka Kenya.
Vingine ni Chuo Kikuu Ndejje kutoka Uganda na kwa upande wa Tanzania
kutakuwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo
cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo
cha Elimu ya Biashara (CBE) na wenyeji Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.
Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stegomena Tax.
0 comments:
Post a Comment