Na Kemeli Arap Kemei,
Father Kidevu Blog-Nairobi
Wananchi wa Kenya wakiwa
katika mitaa mbalimbali wakishangilia kwa furaha ushindi wa Mgombea Urais wa kwa
tiketi ya TNA Uhuru Kenyatta.
Kenyatta ameshinda
Uchaguzi Mkuu wa Kenya kwa kura 6,173,433
dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura 5, 340,546 ikiwa ni
tofauti ya kura 832,887 .
Jumla ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya Urais ni
kura 12,338, 667 kutoka katika majimbo yote ya Uchaguzi 291 huku kura
zilizoharibika zikiwa 108975 na kura halali zikibaki 12,222,980.
Wakenya wapo katika mitaa mbalimbali na vitongoji vya Nchi hiyo
wakishangulia ushindi huo, na wakati huu Maandalizi katika eneo la Bomas
kwaajili ya kutangaza rasmi matokeo hayo yanaendelea ambapo Mwenyrekiti wa Tume
ya Uchaguzi ya Kenya IEBC anataraji kumtangaza Rasmi Uhuru Kenyatta kama
Mshindi wa Urais.
Hii ndio hali halisi ya hivi sasa nchini Kenya lakini kubwa zaidi la kuwapongeza
wakenya wote ni hali ya amani iliyopo katikia miji mbalimbali. Pia Wagombea
ambao wamekubali matokeo hayo huku wengine wakitangaza tangu jana kukubali
kushindwa na kuungana katika kuijenga Kenya moja iliyo na amani na utulivu.
0 comments:
Post a Comment