WACHEZAJI wa Kimataifa wa Tanzania wanaocheza
Soka la Kulipwa Nchini Congo DRC, wanaochezea timu ya TP Mazembe Mbwana Samata
na Thomas Ulimwengu wamewasili nchini jana na kuwahakikishia Watanzania Ushindi
dhidi ya Morocco.
Samata na Ulimwengu wamewasili nchini wakitokea
Nchini Boswana walikokuwa na Timu yao ya TP Mazembe na kuja kuungana na wenzao
katika Kambi ya Timu ya Taifa inayo jinoa dhidi ya Morocco mchezo utakao
fanyika baade mwezi huu.
Akizungumza mara baada ya kuwasili, Mbwana
Samata amesema ushindi dhidi ya Morocco ni lazima, hivyo Watanzania wasiwe na
hofu na timu yao na wao wako tayari kuliongoza jahazi hilo la ushindi.
“Tumekuja kuungana na wachezaji wenzetu wa Timu
ya Taifa, tumekuja kuhakikisha timu yetu inashinda na tuna kila sababu ya
kushinda maana tunacheza Nyumbani,” alisema Samata.
Amesema kuwa wao wako fiti na hawana tatizo
lolote na wanajiunga na kambi usiku huo huo waliowasili na kuanza mazoezi kama
ratiba ilivyo pangwa na hivyo watanzania wajiandae kushangilia ushindi.
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro lager, imeingia kambini tangu juzi
kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Morocco jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars itacheza
mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014
nchini Brazil dhidi ya Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili Machi 24, katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
wanaocheza soka la Kulipwa nchini Congo DRC katika Timu ya TP Mazembe, Thomas
Ulimwengu (kushoto) na Mbwana Samata wakiwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili tayari kwa
kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Morocco.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
wanaocheza soka la Kulipwa nchini Congo DRC katika Timu ya TP Mazembe, Thomas
Ulimwengu (kushoto) na Mbwana Samata wakizungumza na mmoja wa mashabiki wa Soka
nchini Tanzania aliyewalaki walipo wasili
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam jana tayari kwa kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ikiwa ni maandalizi
ya kuikabili Morocco.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
wanaocheza soka la Kulipwa nchini Congo DRC katika Timu ya TP Mazembe, Thomas
Ulimwengu (kulia) na Mbwana Samata wakizungumza na mmoja wa Mfanyakazi wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Haji Mpangachuma (katikati) aliyewalaki
walipo wasili uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana tayari kwa
kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Morocco.
0 comments:
Post a Comment