MO BLOG: Tulishuhudia
uzinduzi wa ‘Ongea na Janet’ tukaanza kuona vipindi vikienda hewani hebu tuweke
wazi yapi mafanikio uliyopata mpaka sasa..?
JANET: Mafanikio
nilianza kuyaona kwenye vipindi 13 tu vya mwanzo ambavyo vilitengeneza ‘Season One’. Nashukuru Mungu ‘Ongea na
Janet’ ilijulikana haraka sana, ikapata watazamaji wengi, ‘comments’ nazo
zikawa nyingi, ‘changes’ zikawa nyingi nikajikuta kila ninapokwenda siitwi tena
Janet naitwa ‘Ongea na Janet’.
Hilo lilikuwa ni fanikio la kwanza kwamba niliondoka kwenye
media muda mrefu na niliporudi nikapokewa vizuri kwa hiyo nawashukuru kwanza
watanzania wenzangu kwa hilo, nawashukuru sana mashabiki wa Janet kwa kunipa
‘love’ ukweli.
Lakini pia fanikio lingine lilikuja kujitokeza ambalo
sikulitegemea kwa kipindi kile lilikuja kama ‘surprise’ kwangu kwani nikiwa sina hili wala line nikapata simu
kutoka MNet-Dstv Nairobi wakaniambia kwamba shoo yangu wameipenda na
wataichukua, wakati huo nikuwa nimesha ‘apply’
siku nyingi sana mpaka nimesahau.
Wakanipa na ‘amount’
nikakubali wakaniuliza unazo ngapi? Wakati huo ndio nimemaliza ‘Season One’ nikawaambia ziko 13
wakasema wangependa kama zingekuwa 26 nikasema sawa nitakaporudi ‘Season Two’ nitawapatia wakakubali.
Hivyo niliporudi ‘Season
Two’ nikawa nimeingia kibiashara zaidi na Dstv wakawa wameni-‘support’
nikaweza kubadilisha set up nzima ya ‘Ongea
na Janet’ na wakanipa hamasa zaidi
na nikapata nafasi ya kuitangaza nchi yangu kwa na kwa sababu naoneka katika
nchi nane (8) tofauti.
Pia nikagundua moja kwa moja kuwa sasa nimeingia kwenye ‘competition’ na watu nane
wanaoziwakilisha nchi zao kwa maana ya kwamba Tanzania iko kwenye ‘competition’
ya ‘talk show’ na nchi nane za
Afrika.
Mashabiki wangu nataka niwaambie kwamba nitajitahidi
kuboresha kazi zangu na natamani Talk Show bora East and Central Africa itoke
Tanzania.
MO BLOG: Unalipi
la kuwaambia watanzania lolote lile sio la fani yako.
JANET: Kinachoniumiza
naona kama amani inataka kupotea nchini mwangu hivyo mimi naomba tu wanaohusika
watusaidie, kwa sababu ukitaka kujua ubaya wa kutokuwa na amani, anzia nyumbani
kwako usipokuwa na amani na mtu unayeishi naye nyumba haikali au siyo.? Hivi
sisi kweli leo tukawe wageni kwa watu? Hii kitu kidogo inaniumiza.
Kusoma Mahojiano yoteBofya
Hapa
0 comments:
Post a Comment