Papa
Francis
Hatimae Jopo la Makardinali 115 wa Kanisa
katoliki wamemchagua Kardinali wa Buenos
Aires kutoka Latin Amerika Jorge
Mario Bergoglio (76) kuwa kiongozi
mpya atakaye chukuwa nafasi ya Papa
Benedict aliyejiuzuli hivi karibuni.
Jorge Mario Bergoglio
ambaye ni Muagrgentina tayari amechagua jina la atakalo litumia katikakipindi
chake cha Uongozi kuwa atatambulika kama Papa Francis.
Jopo
la Makardinali wamemchagua Cardinali kutoka Latin America Cardinal Jorge Mario Bergoglio, kushika wadhifa mpya wa Papa katika uchaguzi uliofanyika kwa mara ya
tano kwa kura zilizopugwa na Makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika kanisa
la Sistine Chapel huko Vatican , Roma.
Maelfu
ya watu walikuwa wamefurika katika eneo la la St. Peters huko Vatican huku
mamilioni wengine wakishuhudia Papa huyo mpya akitangzawa mbele yao.
Papa Francis ni Papa wa Kwanza kuchaguliwa
kutoka Latin America tangu kuanzishwa kwa Kanisa Katoliki Duniani.
Aliwahi pia kutajwa kumrithi Papa John Paul II
wakati wa kumtafuta Papa na akashinda Papa Benedict ambaye amejiuzulu.
0 comments:
Post a Comment