Makamu wa Rais wa Tanzania,
Dk. Mohamed Gharib Bilali, jana aliwasha moto wa kuteketeza silaha ndogo ndogo
ambazo zimekuwa hatari katika jamii ya Watanzania na wana Afrika Mashariki kwa
ujumla kwa silaha hizo zilizokuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria kutumika
katika uhalifu na mauaji ya aina mbalimbali ya watu na wanyapori katika
hifadhi.
Mbali na Makamu wa Rais pia
zoezi hilo lilishuhudiwa na viongozi wengine mbalimbali wa Jumuia ya Afrika
Mashiriki, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania pamoja na Mawaziri kutoka nchi
wananchama wa EAC wanaoshughulika na masuala ya Ulizni na Ushirikiano wa Kimataifa.
Pichani ni matanuru mawili ya
silaha hizo zaidi ya 3000 yakiteketea kwa moto huo uliowashwa na Makamu wa Rais
katika eneo la Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed
Gharib Bilal akipita kukagua matanuru hayo mawili ya kuteketezaea silaha kabla
ya kuyalipua kwa moto.
Balozi wa
Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes ambaye nchi yake
kupitia shirika la GIZ limekuwa likifadhili shughuli mbalimbali za Jumuia ya Afrika
Mashariki akikagua matanuru hayo.
Makamu wa Rais Dk.
Mohamed Gharib Bilal akivuta kamba maalum kufyatua baruti iliyowasha moto
katika matanuru hayo ya silaha na kuyateketeza.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed
Gharib Bilal akipokea mkono wa shukrani kutoka kwa Katibu Mkuu wa EAC, Balozi
Dk. Richard Sezibera mara baada ya kulipua matanuru hayo. Katikati yao ni
Balozi wa Ujerumani nchini, Klaus-Peter Brandes na kulia ni Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani wa Tanzania, Pereira Silima.
Viongozi wakiangalia moto huo ukiteketeza
Hiki ndio kizazi hasa cha kuelimishwa juu ya matumizi mabaya ya silaha na kujiepusha na vurugu ziletazo maafa.
0 comments:
Post a Comment