Na Anna Nkinda-Sumbawanga
Taaasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) imeikabidhi hospitali ya mkoa wa Rukwa - Sumbawanga kontena la urefu wa futi 40 lenye mitambo ya kisasa na vifaa vya huduma ya afya ilivyochangiwa na Shirika linayoshughulika na utoaji wa huduma za kibinadamu la Project C.U.R.E la nchini Marekani vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba .
Taaasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) imeikabidhi hospitali ya mkoa wa Rukwa - Sumbawanga kontena la urefu wa futi 40 lenye mitambo ya kisasa na vifaa vya huduma ya afya ilivyochangiwa na Shirika linayoshughulika na utoaji wa huduma za kibinadamu la Project C.U.R.E la nchini Marekani vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba .
Makabidhiano hayo
yalifanyika jana katika viwanja vya Hospitali hiyo ambapo Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Taasisi hiyo aliwataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kuvitunza na kuvitumia
vifaa hivyo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi na si
vinginevyo.
Akiongea na wananchi wa
mkoa huo pamoja na wahudumu wa afya waliohudhuria hafla hiyo Mama Kikwete alisema kuwa kupatikana kwa
vifaa hivyo ni kutokana na changamoto mbalimbali alizokuwa ameelezwa katika ziara zake za mikoani ambazo
zilimpa msukumo mkubwa wa kwenda mataifa
mbalimbali kwa kuwa aliona anao wajibu
wa kufanyia kazi matatizo aliyoelezwa yakiwemo ya upungufu wa vifaa vya kutolea
huduma za afya.
“Bila ya shaka yoyote vifaa na mitambo
ninayoikabidhi leo vitafanya kazi kubwa katika kutoa huduma bora zaidi ya
afya na kuokoa maisha ya wananchi wetu
katika hospitali ya Sumbawanga”, alisema Mama Kikwete.
Akisoma taarifa ya
Hospitali hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. John Gurisha alishukuru kwa mitambo na
vifaa tiba walivyopewa na kuahidi
kufanya kazi kwa uwezo wao wote ili kufanikisha azma ya kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Dk. Gurisha alisema kuwa hospitali hiyo inahudumia wakazi
wa mkoa huo na Katavi wapatao 1,760,639
na wanatoa huduma za tiba, kinga na ushauri wa kitaalamu. Inauwezo wa
kuwa na vitanda 450 na wastani wa kulaza wagonjwa 300 kwa siku lakini kwa sasa inavitanda 270 na inalaza
wagonjwa 160 kwa siku.
“Baadhi ya changamoto
tunazokabiliana nazo ni upungufu wa watumishi wenye ujuzi, ucheleweshaji wa
matengenezo ya vifaa mara linapotokea tatizo na hivyo kusababisha wagonjwa
kutopata huduma inayostahili kwa wakati na
imani na mila potufu katika jamii imekuwa ni kipingamizi kikubwa katika
utoajia wa huduma bora za afya kwani wagonjwa wengi wamekuwa wakichelewa kufika
hospitali mpaka wapitie kwanza kwa waganga wa jadi”, alisema Dk. Gurisha.
Aliyataja mafanikio
waliyoyapata kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kuwa ni kuajiri madaktari
saba na wauguzi 11, wamepata wateknolojia watano wa maabara kutoka Taasisi ya
Benjamini William Mkapa, wamejenga chumba cha kuhifadhi dawa za chanjo, wodi ya
wagonjwa wa akili, wodi moja ya daraja la kwanza , maabara ya kisasa kwa msaada
wa Serikali ya Marekani, chumba cha upasuaji na wodi ya wazazi.
Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Project
C.U.R.E Dk. Abdul Kimario alimpongeza Mke wa Rais kwa
jitihada alizozifanya kwa muda mrefu za kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vimefika
nchini na kuwaomba watanzania wamuunge mkono kukabiliana na upungufu wa vifaa
tiba mahospitalini kwani jitihada alizofanya ni kubwa na amepanda mbegu ambayo itaota kwa miaka mingi.
Dk. Kimario alisema kuwa kabla ya kutumwa
kwa vifaa hivyo nchini alikuja kufanya tathimini na kuangalia ni Hospitali gani
inamahitaji makubwa zaidi na kugundua kuwa hospiatali za Rukwa (Sumbawanga) na
Lindi zinamahitaji makubwa ukilinganisha na zingine.
“Shirika
letu linafanya kazi katika nchi 125 zinazoendelea, tumieni nafasi hii kwa
kushirikiana na WAMA ili muweze kupata vifaa tiba katika Hospitali zenu za
wilaya na mikoa kwani vifaa tunavyo vingi na baadhi ya nchi tulizozipelekea vifaa ni
Jamuhuri ya watu wa Kongo, Malawi, Nigeria, Ghana, Tunisia, Mauritania,
Ethiopia, Sudani, Kenya na Uganda”, alisema Dk. Kimario.
Kupatikana kwa vifaa hivyo ni jitihada ya Mama Kikwete
za kuhakikisha kuwa vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinapungua hapa
nchini kutokana na hilo Shirika la Project C.U.R.E ilifanya
harambee ya kumuunga mkono mwezi wa nne mwaka 2011 na kumchangia makontena matano ya vifaa vya afya vyenye
thamani ya dola za kimarekani milioni tatu sawa na shilingi bilioni 4.5 za
kitanzania.
Kabla ya
kutumwa kwa vifaa hivyo wataalamu kwa
afya kutoka Project C.U.R.E walikuja
nchini kufanya tathimini ya vifaa vinavyohitajika katika Hospitali na
Kliniki ambazo zilipendekezwa na wizara
ya Afya na Ustawi wa jamii ili kutambua mahitaji mahususi,
tecknolojia na nishati iliyopo kwani
kila kifaa kilichotolewa kinahitajika mahali husika na kinaweza kutumika katika mazingira na
tecknolojia iliyopo.
Baadhi
ya mitambo
iliyokabidhiwa ni mashine ya Ultra sound, vifaa vya X-ray, mitambo na
vitanda maalum cha ICU
kwajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa mahututi, vifaa vya upasuaji mkubwa
na
mdogo, vifaa vya upasuaji na tiba ya macho ya kisasa (laser), mitambo,
viti na vifaa vya huduma ya tiba ya
kinywa na meno, vifaa vya tiba, mitambo na tiba ya mgongo na mifupa na
taa ya meza maaluma ya upasuaji na mashine ya usingizi (anaethetic
machine)
Kontena moja lenye mitambo na vifaa tiba limeshakabidhiwa kwa
Hospiali ya mkoa ya Lindi Sokoine na mengine yatapelekwa katika Hospitali za mikao ya Simiyu, Tabora, Tumbi na
Mtwara .
0 comments:
Post a Comment