***
Na Mwandishi wa Father Kidevu Blog, DSM.
Licha ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuzuia
maandamano ya Waumini wa Dini ya Kiislam, baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni
Waumini wa Dini hiyo katika maeneo ya Buguruni, Malapa na Kariakoo wamefanya
maandamano hayo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi kupitia Vikosi vya Kutulia
Ghasia-FFU-limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya waandamanaji
hao waliokuwa wamebeba Mabango na Mawe kwenye Mifuko katika Mitaa ya Malapa
pamoja na Kariakoo.
Katika tukio hilo Uhuru FM imeshuhudia Maduka mbalimbali yakiwa
yamefungwa katika Mitaa ya Kariakoo kutokana na maandamano hayo ya watu
wanaodaiwa kuwa Waumini wa Dini ya Kiislam.
Waumini hao wanashinikiza Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa
Mashitaka-DPP-kumwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya ya Waislam Shekh PONDA
ISA PONDA ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
0 comments:
Post a Comment