Basi jipya la Taifa Stars ambalo limenunuliwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni hiyo
kwa timu ya Taifa. Basi hilo linatarajiwa kukabidhiwa Februari 21.
******
Hatimaye basi la Timu ya Taifa, Taifa Stars
lililokuwa likisubiriwa kwa hamu sasa limewasili na liko tayari kukabidhiwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) ili
Taifa Stars iweze kulitumia.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia
ya Kilimanjaro Premium Lager, inayodhamini Taifa Stars, George Kavishe alisema
hii ni katika malengo yao ya kuinua hadhi ya timu ya Taifa ambayo kwa sasa
imeonesha kiwango cha hali ya juu.
“Wakati tukichukua udhamini wa timu ya Taifa
moja ya malengo yetu ilikuwa ni kuinua hadhi ya timu hii na mojawapo ya vitu
tulivyoahidi ni kuinunulia basi la hadhi,” alisema Bw Kavishe.
Alisema basi hilo aina ya Yutong lenye thamani
ya zaidi ya Shilingi milioni 200, ni kubwa na la kisasa kabisa lenye uwezo wa
kubeba abiria 50 pamoja na dereva na kuwa lina nafasi kubwa kutoka kiti kimoja
hadi kingine hivi kuwafanya wachezaji wakae kwa raha zaidi wanaposafiri.
“Basi hili ni athletic coach na ni jipya kabisa,
limetengenezwa mahususi kwa wanamichezo kwani lina nafasi kubwa chini ya kubeba
vifaa vya michezo na mizigo mingine yeye uzito wa hadi tani tatu,” alisema Bw.
Kavishe.
Aliendelea kusema kuwa basi hilo ni imara kwani
chasis yake ni 4x2, injini yake ni aina ya 300 HP Cummins, ina retarder
ya umeme na breki aina ya ABS, TV mbili za kisasa, muziki wa nguvu wenye spika
nane, milango na mabuti ya kisasa, friji mbili na kiyoyozi cha nguvu.
Kwa mujibu wa Bw. Kavishe basi hili linatarajiwa
kukabidhiwa kwa Taifa Stars Februari 21 katika hafla itakayofanyika katika
makao makuu ya TBL Ilala Jijini Dar es Salaam na itahudhuriwa na wadau
mbalimbali wa soka nchini na wageni wengine.
Baada ya kukabidhiwa kwa Taifa Stars basi hilo
linatarajiwa kuzunguka katika mitaa mbalimbali ya JIji la Dar es Salaam ili
wananchi walione na wapige nalo picha za kumbukumbu.
“Hii ni zawadi ya watanzania kwa timu ya Taifa
kwani ndio wanatuwezesha kufanya mambo yote haya…kadri wanavyozidi kutuunga
mkono kwa kunywa bia yetu ya Kilimanjaro Premium Lager ndivyo na sisi tunapata
fedha za kuidhamini timu yetu ya Taifa,” alisema.
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ilianza
kuidhamini Timu ya Taifa tangu mwezi Mei mwaka jana kwa kuwekeza zaidi ya
bilioni mbili kwa mwaka kwenye timu hii kwa muda wa miaka mitano.
Moja ya masuala ambayo yamo kwenye mkataba kati
ya TBL na TFF ni ununuzi wa basi mpya ya Taifa Stars jambo ambalo TBL
imefanikisha ndani ya mwaka mmoja wa udhamini wake.
Mpaka sasa TFF imeonyesha kuridhishwa na
udhamini mnono wa Kilimanjaro Premium Lager kwani shirikisho hilo lina uwezo wa
kufanya mipango ya muda mrefu zaidi kwa uhakika.
Udhamini wa Kilimanajro Premium Lager ndio
mkubwa kabisa ambao TFF imewahi kupokea kutoka kwa kampuni au shirika lolote
nchini kudhamini mpira.
0 comments:
Post a Comment