kurugenzi Mkuu wa shirika la hifadhi za wanyama Nchini (TANAPA) Alan
Kijazi akimkabidhi zawadi ya mpira mtoto aliyeshinda juzi jijini
Arusha katika shindano la mchezo wa miguu ambapo shirika hilo liliweza
kujumuika na familia zao(family day) katika kukaribisha mwaka mpya huku
michezo
mbalimbali zikitawala pamoja na burudani ya muziki ikichukua nafasi
yake.
*****
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Wadau mbalimbali
wametakiwa kuunganisha nguvu ya pamoja ili kuhakikisha jamii inapata maji safi
na salama kwa kuvitunza na kuboresha vyanzo mbalimbali vya maji vilivyopo
katika hifadhi zetu
Kauli hiyo
ilitolewa jijini hapa juzi, na Kiongozi wa mradi wa Sumit on the Sumit Kenna
Zemedkun kwa waandishi wa habari wakati wa tukio maalumu la kulipokea kundi la
watu maarufu kutoka Nchini Marekani walioshiriki kupanda mlima Kilimanjaro
Meneja mahusiano
wa shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Pasco Shelutete alisema kwa kutambua umuhimu wa vyanzo vya maji katika
mlima huo wamekuwa wakifanya jitihada za maksudi katika kupambana na vitendo
vya uharibifu wa mazingira ndani ya mlima huo ikiwemo utowaji wa elimu kwa
jamii,
Kenna alisema
kuwa lengo la ziara yao nyenye kaulimbiu Sumit of the Sumit,ni kujenga na
kuibua uelewa kwa wananchi kuhusu janga la upatikanaji wa maji safi na salama
kwa kutumia watu maarufu wakiwemo wasanii na wanataaluma waliobobea
Kwa kupitia mradi
huo kundi hilo liko tayari kushirikiana na taasisi yeyote itakayo jitokeza
kutoa huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi
0 comments:
Post a Comment