Mabingwa wa soka Tanzania bara, Simba jana
walipoteza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Jeshi la Oman kwa
magoli 3-1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Qaboos complex jijini Muscat.
Bao pekee la kufutia machozi la Simba liliwekwa kiamiani na mshambulaiji wake Haruna Moshi 'boban' katika kipindi cha pili.
Mwenyekiti wake Ismail Aden Rage alikuwa
jukwaani pamoja na viongozi wengine wa simba, mdhamini wa safari hiyo Rahma Al Kharusi
na Musleh Rawahi pamoja na kocha Talib Hilal wakiishuhudia simba ikizama mbele ya
wanajeshi hao ambao kikosi chao kina wachezaji tisa wanaocheza timu ya taifa ya oman.
Picha
kwa Hisani ya Saleh Ally wa Champion-GPL.
Simba walipofunga goli.
0 comments:
Post a Comment