Nafasi Ya Matangazo

January 08, 2013

Mahmoud Ahmad,Arusha

SAKATA la baadhi ya wananchi pamoja na wanasiasa kupinga usafirishwaji wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda jijini Dar es salaam limezidi kuchukua sura mpya baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM(Uvccm) mkoani Arusha,James Ole Milya kutamka ya kwamba serikali ina lengo la kuufanya mkoa wa Mtwara ubaki kuwa katika lindi la umaskini wa kutupwa.

Hatahivyo,Milya ambaye kwa sasa amehamia Chadema amemtaka Rais Jakaya Kikwete pamoja na baraza lake la mawaziri kuwaonea huruma wakazi wa Mtwara huku akisisitiza ya kuwa wakumbuke maisha ya miaka 50 ijayo kuanzia sasa na si kujijali peke yao wakati wakiwa madarakani.

“Kitendo cha serikali kutaka kujenga kiwanda cha gesi Bagamoyo ni kutaka kuumaliza mkoa wa Mtwara ubaki kuwa maskini wa kutupwa hilo halikubaliki”alisema Ole Milya

Akihojiwa na mwanahabari hii jana jijini hapa,Ole Milya alisema kuwa Mungu hakukosea kubariki rasilimali mbalimbali katika maeno mengi hapa nchini na ndiyo maana hata Mtwara kumevumbuliwa rasilimali kama gesi.

Alisema kuwa serikali ina uwezo wa kujenga kiwanda cha gesi mkoani humo na kasha kuweka utaratibu mzuri wa kusafirisha gesi hiyo hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema kuwa kuna faida nyingi kwa kiwanda hicho kujengwa mkoani humo kama huduma za afya kuboreshwa,elimu pamoja na miundombinu hivyo alisisitiza umuhimu wa kujengwa kiwanda mkoani Mtwara.

Alisisitiza kuwa waziri wa nishati na madini,Sospether Muhongo hapaswi kuwa na fikra mgando kutoa kauli za kejeli kwa wakazi wa Mtwara huku akimtaka afikirie maisha ya watanzania katika kipindi cha miaka 50 ijayo wakati atakapokuwa hayuko madarakani.

Alisema kuwa tatizo kuu la msingi linaloikabili serikali ya Rais Kikwete ni baadhi ya watumishi wake kupenda asilimia kumi katika kila mradi huku akidai tabia hiyo ndiyo inaua nchi.

Hatahivyo,alionya na kutoa ushauri kwa wakazi wa Mtwara kuwa wanapaswa kutambua ya kwamba rasilimali ya gesi iliyopo ndani ya mkoa wa wao inapaswa kuwanufaisha watanzania wote.

“Wananchi wa Mtwara ni lazima watambue ya kuwa rasilimali ya gesi iliyopo pale ni rasilimali ya taifa lote watu wote wanapaswa kunufaika nayo ila kipaumbele kiwekwe Mtwara”alisisitzia Ole Milya
Posted by MROKI On Tuesday, January 08, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo