Nafasi Ya Matangazo

January 02, 2013

Na Fadhili Athumani, Moshi
WAKAZI wa Mtaa wa Dobi, Kata ya Njoro, Wilaya ya Moshi mjini, Mkoani Kilimanjaro, walijikuta wakianza Mwaka kwa majonzi baada ya kijana Abdalla Mussa (22), kukutwa akiwa amekufa, Nyumbani katika tukio linalodhaniwa kuwa ni ya kujinyonga.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana majira ya saa saba mchana ambapo Father  Kidevu Blog iliweza kufika katika eneo la tukio na kukuta maiti ya Marehemu ikiwa bado imening’inizwa kwa kipande cha kitenge kwenye Nyumba Bovu lililo karibu na Nyumba ya Mzazi wa Marehemu.

Marehemu kwa mujibu wa Mama Mzazi, Hawa Athumani, alikuwa anasumbulia na Malaria ambapo wiki mbili kabla ya tukio hilo, Marehemu alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.

“Mwanangu alikuwa anaumwa Malaria na Baada ya kumpeleka pale Mawenzi madaktari walisema kuwa Malaria imepanda kichwani, alitibiwa na ijumaa iliyopita tuliruhusiwa kurudi Nyumbani lakini jana (juzi) alianza kulalamika kuwa kichwa kinauma,” alisema Hawa.

Alisema kuwa siku ya tukio, Marehemu aliamka akiwa mzima kabisa na hadi tukio la kujinyonga linatokea alikuwa mzima kabisa na wala hakuonesha dalili zozote za kutia wasiwasi na kuongeza kuwa baadae muda wa saa Saba mchana, akiwa ameenda sokoni kufanya maandalizi ya sikuukuu, mwanae wa kiume, alimpigia simu na kumjulisha kuhusu tukio hilo.

Kwa upande mdogo wa Marehemu ambaye alizungumza na Gazeti kwa masharti ya jina lake kutotajwa Gazetini alisema kuwa Kaka yake muda mfupi kabla ya kufariki dunia, alikuwa anafanya fujo kwa majirani na kutamka wazi kuwa lazima, siku patokee msiba lakini kutokana na kufahamu hali yake maneno yake hawakuyachukulia kwa uzito mkubwa.
 
“Kaka alikuwa tayari kashajua kufa kwake, alianza kufanya fujo na kupiga watu ovyo na kusema kuwa siku ya leo lazima mtu afe, sasa sisi kutokana na kufahamu hali yake wala hatukuchukulia maneno yake siriazi tukaona labda ni maneno tu.

“ Baadaye kama mwendo wa saa sita na nusu mchana nilishangaa kuona utulivu usio wa kawaida na nilipoingia chumbani kwake sikumkuta, tukaanza kumtafuta, kidogo mtoto wa nyumba ya jirani akaja na kuniambia ameona kitu kimengini akwenye ile nyumba bovu pale, tulienda kuangalia ni nini na kukuta kaka amekufa,” alisema Mdogo huyo wa Marehemu.

Akizungumza tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa huo, Lucy Peter Asenga, alisema kuwa, mara baada ya kupata taarifa za msiba huo, aliwasiliana na Jeshi la Polisi kuomba msaada lakini cha kushangaza pamoja na kutoa Taarifa mapema, msaada walikuja kuupata masaa mawili baada ya kutoa Taarifa.

Akionesha masikitiko yake katika utendaji na ushirikiano wa Jeshi hilo mwemnyekiti huyo alisema kama utaratibu wa kutoa msaada wa Jeshi la polisi hautabadilishwa itafikia muda ambapo wananchi watatafuta msaada kwengine au kujichukulia hatua wenyewe jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Nchi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio Hilo, Kamanda wa Polisi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema mwili wa Marehemu tayari umaeshahidhiwa katika chumba cha Kuhifadhia Maiti ya Mawenzi na kuongeza kuwa Uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho kinaendelea.

Kamanda Boaz alitumia Nafasi kuwataka wananchi kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha huku akito pole kwa Famila ya Marehemu kwa Msiba huo uliowakuta.


Posted by MROKI On Wednesday, January 02, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo