Na Abdulaziz Video.
WATU Saba akiwemo askari polisi mmoja wameuawa katika vurugu
zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara, zikiwa zimebeba sura ya
kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.
Muuguzi wa zamu hospitali ya wilaya
ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu amethibitisha kupokea maiti za watu
saba.
Majeruhi ambao idadi yao haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya
misheni ya Ndanda kwa matibabu na hali bado ni tete Vurugu kubwa
zilianza majira ya saa 4 asubuhi leo baada ya polisi waliokuwa wakiendesha
pikipiki kumgonga mtu na kukataa kutoa ushirikiano,Hata hivyo hoja
hiyo ilihamia kwenye gesi na kundi la vijana mara moja walivamia nyumba
ya mbunge wa Masasi, Mariam kasembe na kuiwasha moto, pamoja na magari
mawili.
Aidha vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdallah na
kuiteketeza kwa moto,kabla ya kuivania ofisi ya CCM wilaya na kuichoma
moto pamoja na magari matatu.Hasira za wananchi hao zilifika kituo
kidogo cha polisi kilichopo Mkuti na kukichoma moto, baadae walichoma
moto magari matano ya halmashauri ya wilaya.
Pia walichoma moto ofisi
ya elimu ya halmshauri ya wilaya Masasi vijijini, kabla ya kuichoma
ofisi ya maliasili.
Polisi kutoka maeneo mbalimbali yandani na
nje ya mkoa inadaiwa walitumia risasi za moto na kusababisha vifo vya
watu Sita huku polisi akidaiwa kuuawa kwa kupigwa na wananchi….
0 comments:
Post a Comment