Chanzo
chetu cha Habari kutoka Kibiti kinaipasha Father Kidevu Blog kuwa kijana
aliyefariki kutokana na kipigo hicho ni Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika
wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili.
Habari
zaidi zinapasha kuwa hivi sasa wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari
Polisi hao zilizopo jirani na kituo hicho, licha ya juhudi za Polisi
kuwatawanya kwa mabomu kuendelea kufanyika.
Aidha
wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini,
Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama
kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.
Hali
inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada
za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya umati huo
wa watu.
Father
Kidevu Blog, ipo eneo la tukio na itakuletea taarifa zaidi na picha maana hivi
sasa ni milipuko ya mabomu tu kwenda mbele.
0 comments:
Post a Comment