Mkurugenzi
wa Fullshangweblog.com Bw. John Bukuku kushoto akipokea tuzo hiyo
kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki katika
maonyesho ya World Travel Market (WTM)Nchini Uingereza mwezi Oktoba
mwaka huu katikati ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utaii Tanzania TTB Bw.
Geofrey Meena.
*****
Mwaka huu Fullshangwe imefanikiwa
kupata Tuzo ya kutangaza utalii wa ndani wa Tanzania kimataifa mwaka
2011 nchini Uingereza inayoitwa TANZANIA TOURISM BOARD WEB TRAVEL
MAGAZINE AWARD 2011, Fullshangweblog.com kupitia kwa mkurugenzi wake
Bw. John Bukuku ilipokea tuzo hiyo katika maonesho ya utalii ya
kimataifa ya dunia World Travel Market (WTM) yaliyofanyika katika
eneo la Exel jijini London nchini Uingereza kuanzaia Oktoba 5 mpaka 8
2012, ambapo Fullshangweblog.com ilikuwa moja ya makampuni yaliyoshiriki
katika maonyesho hayo katika kupasha habari.
FULLSHANGWEBLOG.COM inaushukuru
uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inayoongozwa na Mkurugenzi
Mwendeshaji Dk. Aloyce Nzuki, Mkurugenzi wa Masoko Devotha Mdachi ,
Meneja Masoko Bw. Geofrey Meena na wafanyakazi wote wa bodi hiyo,
pamoja na wadau wake wote kwa kutambua mchango wa FULLSHANGWE.BLOG kama
Web Magazine iliofanya kazi nzuri ya kutangaza utalii wa ndani mwaka
2011 na kuitukukia tuzo hiyo, ninawashukuru sana kwani maana ya tuzo hii
ni kwamba tunamaliza mwaka 2012 kwa mafanikio.
Kuna baadhi ya mambo niliyokumbana
nayo katika kazi zangu za kila siku ” Kuna matukio mengi niliwahi
kukutana nayo katika shughuli zangu za kutafuta habari mengine yalikuwa
ni ya kukatisha tamaa sana, lakini sikukata tamaa niliendelea kukaza
buti kadiri mungu alivyonijalia, Mengine yalikuwa ni ya mafanikio yenye
kutia moyo.
Katikapitapita yangu ya kazi “Kuna
wakati marafiki zangu wa karibu walinikatisha tamaa na kuniuliza kwamba
ninafanya nini mbona sieleweki hasa wakati nilipojitambulisha katika
mikutano mbalimbali kwamba nawakilisha WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM. wengi
hawakunielewa hata kidogo nini ninachokifanya, hata hivyo niliendelea na
juhudi zangu mpaka walipoanza kutambua na kuelewa kwamba nilikuwa
nafanya jambo fulani zuri”
Siku moja nilisafiri kuelekea
nyanda za juu kusini mkoani Iringa nilifika katika wilaya Mufindi
Mafinga nilikutana na kisa ambacho pia nilikiripoti kwenye mtandao, kisa
hiki kilikuwa hivi.
MAPANDA HOTEL WANASEMA LAPTOP COMPUTER INAKULA UMEME KULIKO PASI NA FRIJI!
Nimeingia katika hoteli hii ya Mapanda Hotel and Guest House mjini Mafinga ili niweze kupata kifungua kinywa lakini pia niweze kufanya kazi zangu kwenye kompyuta yangu ya mkononi, ukweli ni kwamba sikupata kifungua kinywa wala kufanya kazi yoyote, Kilichonipoza ni kutumia Kompyuta yangu (Laptop) Meneja wa Hoteli hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alinifuata na kuniambia kwamba siwezi kuendelea kutumia kompyuta yangu kwa kuwa inakula sana umeme ni sawa tu na friji au pasi ya umeme, hivyo ningeweza kumaliza umeme wao wa LUKU, nikajaribu kubembeleza lakini meneja huyo alinikatalia kabisa..
Binafsi sikujali sana wala
sikukubaliana na hoja yake manake nilijua kwamba umande na umbumbumbu
umewajaa kwenye ubongo wao katika teknolojia ya Kompyuta hivyo kwao wao
Kompyuta ya mkononi au Laptop ni sawa usiku wa giza, Ikabidi niondoke
hapo lakini bahati nzuri nikapata Internet Cafe inayoitwa 3A Traders
Internet Cafe hapo nikafanya kazi yangu vizuri kabisa.
Nawatahadharisha ndugu zangu mnaotaka kuja na kompyuta zenu hapa Mafinga msijisumbue kwenda hapo Mapanda Hotel kwani yanaweza kuwapata yalionipata mimi.
MATUKIO YA KUKUMBUKWA
Kati ya matukio ambayo ni ya kumbukumbu kubwa ni tukio la kuzama kwa meli Septemba 10, 2011 ambalo mtandao wa Fullshangweblog.com uliripoti kwa ufupi na kuvuta hisia za watembeleaji wengi.
Kati ya matukio ambayo ni ya kumbukumbu kubwa ni tukio la kuzama kwa meli Septemba 10, 2011 ambalo mtandao wa Fullshangweblog.com uliripoti kwa ufupi na kuvuta hisia za watembeleaji wengi.
Ripoti ilikuwa hivi “MELI ya Spice
Islander imezama usiku wa kuamkia leo ikiwa safarini kuelekea Pemba
ikitokea bandari ya Malindi Unguja.
Meli hiyo inasemekana ilikuwa na abiria wapatao 610 ambapo juhudi za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo bado zinaendelea hivi sasa.
Akizungumzia ajali hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku.
Haji Ussi amesema meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimaye kuzama kabisa”.
Lakini pia tukio lingine
lililovuta hisia za watembeleaji wengi lilikuwa ni kifo cha Mwigizaji
Maarufu nchini Marehemu Steven Kanumba watu wengi walikuwa wakitembelea
mtandao ili kupata taarifa mbalimbali juu ya msiba huo.
NINAJISIKIA VIZURI KUWA BLOGGER
Nimekuwa nikifurahia kazi yangu na kuipenda sana kwani katika kazi yangu hii ya kupasha habari imenikutanisha na watu wengi maarufu, wasio maarufu lakini muhimu katika jamii, wakati mwingine ninaposafiri katika mikoa mbalimbali na vijiji au nje ya nchi, kitu kikubwa kinachonifurahisha ni matukio halisi ninayokutana nayo, kwani nakutana na habari mabazo zinagusa hisia za wasomaji wa mtandao na pia zinanifanya kujifunza mambo mengi yanayotokea duniani. Pia napata habari zenye uhalisia wa maisha ya mtanzania na matukio yenye kuvuta hisia kwa wasomaji.
Jambo ambalo linanifanya nijisikie
vyema zaidi ninapopata nafasi ya kupiga picha na kuandika habari za
kijamii kutoka vijijini katika mikoa mbalimbali na mataifa mbalimbali
hii ni kutokana na mvuto wa picha na habari zenyewe lakini pia ninapata
changamoto za kimawazo na jinsi ya kujikwamua katika maisha ya kila
siku.
SHUKURANI KWA WADAU
Mwisho ninawashukuru wadau wote walionifikisha hapa kwa njia yoyote ile mafanikio ya mtandao wa FULLSHANGWEBLOG.COM si kwa juhudi zangu binafsi, bali pia ni juhudi za wadau wote ambao tulishirikiana nao na tunaendelea kushirikiana nao kwa moyo wa dhati, ni matumaini yangu kwamba tutaendelea kushirikiana kwa karibu ili tuweze kuendeleza juhudi za kujenga nchini yetu nzuri ya Tanzania na kupasha habari zaidi kadiri tutakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu katika mwaka ujao wa 2013.
Mwisho ninawashukuru wadau wote walionifikisha hapa kwa njia yoyote ile mafanikio ya mtandao wa FULLSHANGWEBLOG.COM si kwa juhudi zangu binafsi, bali pia ni juhudi za wadau wote ambao tulishirikiana nao na tunaendelea kushirikiana nao kwa moyo wa dhati, ni matumaini yangu kwamba tutaendelea kushirikiana kwa karibu ili tuweze kuendeleza juhudi za kujenga nchini yetu nzuri ya Tanzania na kupasha habari zaidi kadiri tutakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu katika mwaka ujao wa 2013.
Lakini naomba nitaje baadhi ya
taaisisi, mashirika na wadau kadhaa waliotusaidia na wanaendelea
kutusaidia kwa kututumia habari na matukio mbalimbali, ninatoa shukurani
kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Idara ya Habari Maelezo,
Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Kitengo cha habari Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kitengo cha Habari Ofisi ya Makamu wa Rais, Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB),Kitengo cha habari Ofisi ya Bunge, Vitengo vya habari
Katika Wizara mbalimbali, Mashirika, Makampuni binafsi, Idara za
serikali na wadau mmoja mmoja waliotusaidia kupata habari mbalimbali
muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
Nitakuwa siyo mwingi wa fadhila
kama sitawashukuru kaka zangu Muhidin Issa Michuzi na Maggid Mjengwa,
kaka zangu walionitangulia kwa umri na kazi ya kublogu ninawashukuru kwa
ushauri wo ninaoweza kuuita maalum, pia kwa msaada wao katika
kunielekeza mambo mengi juu ya uelewa wa kublogu, ambao nimekuwa
nikipewa wakati wote, nashukuru sana kaka zangu naomba tuendelee na moyo
huohuo na mungu atutangulie katika yote, Lakini pia niwashukuru
mablogger wenzagu Michuzijunior wa Jiachieblog au Ahmed Michuzi kama
anavyojulikana, Mroki Mroki, Zainul Nzige, Carthbert Kajuna, Othman
Michuzi, Abdalla Mrisho, Josephat Lukaza , Muhidin Sufian na Mwanamke
blogger mkongwe Mamaa Shamimu Mwasha wote ninawapenda sana.
Mwisho napenda kumshukuru dada
yangu, mwandishi wetu na mpiganaji Gladness Mushi wa FULLSHANGWEBLOG.COM
mkoani Arusha, ninakushukuru dada yangu kwa kuipigania FULLSHANGWEBLOG
na kuitambulisha kwa nguvu mkoani Arusha kutokana na habari nyingi za
kijamii ambazo umekuwa ukizituma kutoka huko, tuko pamoja na FULLSHANGWE
inakuangalia kwa macho mawili Mungu akubariki sana na uwe na afya njema
ili tuendeleze kazi
0 comments:
Post a Comment