Mwenyekiti
wa CHANETA, Anna Bayi akiwa Mwenyekiti wa wake za viongozi, Germina
Lukuvi mara baada ya timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens) iliporejea
nchini na Kombe la Michiuano ya Kimataifa iliyofanyika nchini
Siangapore.
Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens’ wakiwasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam leo wakitokea Singapore walikokuwa wakishiriki michuano ya
Kimataifa na kutwaa Kombe la michuano hiyo.
Mlezi
wa Chaneta kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Ain Sharif
akikabidhi kitita cha sh. 500,000 ikiwa ni kama zawadi kwa timu hiyo
baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa yaliyofanyika
Singapore na Taifa Queens kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Wachezaji
na viongozi wa timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Quees) wakiwa katika
picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili leo kwenye uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea nchini Singapore.
*********
Na Mwandishi Wetu
TIMU
ya taifa ya Netiboli ya Tanzania ‘Taifa Queens’ imerejea kwa kishindo
leo baada ya kushiriki na kutwaa Kombe la michuano ya Kimataifa
iliyokuwa ikifanyikia Singapore barani Asia.
Taifa
Queens ilitwaaa ubingwa huo baada ya kuingia fainali ikiwa na pointi 10
ikicheza na timu ya Malasia iliyokuwa na pointi 4 ambapo ilifanikiwa
kuifunga magoli 45-38.
Akizungumza
baada ya kurejea, Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA),
Anna Bayi alisema maandalizi ni kitu kizuri sana, anaamini kocha aliwapa
wachezaji mbinu za kutosha hadi kupelekea ubingwa huo.
“Hii
imetusaidia sana maana kocha mwenyewe ni kijana hivyo anambinu za
kisasa kitu kilichotusaidia wakati tukiwa ugenini, hakuna kitu kizuri
kama kupigiwa wimbo wa taifa lako ukiwa ugenini huku wazungu ambao ni
wenyeji wa mashindano hayo wakiwa penbeni,” alisema Bayi.
Kwa
upande wake Kocha wa Taifa Queens, Mary Waya alisema mashindano
yalikuwa ni magumu anawapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo ambao
umemuweka pazuri yeye pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.
“Kila
kitu unatakiwa umtangulize mungu, akili, na nguvu ndio zinafuata
naimani wachezaji wangu walikuwa makini na kujua nini wamekifuata huko,
akili ni kitu cha muhimu ukiwa mchezoni hivyo mimi sina la kusema zaidi
ni kumshukuru mungu kwa ushindi tulioupata,” alisema Kocha huyo ambaye
ni Mmalawi.
Kocha
huyo alisema amefurahishwa na ushindi huo na kwamba kwasasa anajipanga
kuifua timu hiyo kwaajili ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia.
Naye
Nahodha wa timu hiyo, Lilian Sadolin alisema anamshukuru mungu kwa
ubingwa huo pia Watanzania wanatakiwa kuendelea kuwapa sapoti katika
mashindano mbalimbali.
“Wakati
tunaondoka niliwaahidi Watanzania lazima turudi na ushindi, sisi
ubingwa tushaapata kabla hatujaenda kule tulienda kutimiza wajibu,
naimani tuliwazidi mbinu unapokuwa uwanjani unatakiwa kuwa na mbinu za
ziada hivyo tunamshukuru mungu kwa ushindi tulioupata,” alisema Lilian.
mmejitahidi jamani angalau tutasemea hata hiyo lakini fb nooooooooooooooooooooooooooooooo
ReplyDelete