Nafasi Ya Matangazo

December 23, 2012


Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema amewaahidi wapiga kura wake kutoendelea na siasa za maandamano na badala yake sasa ni kazi tu na mijada la malalamiko yote ni katika vikao.

Akihutubia wananchi, alisema yuko tayari kuwatumikia Wana-Arusha huku akiahidi kuwa hatoandamana tena, bali madai na kero zake atazielekeza kwenye vikao ndani ya Halmashauri.
 Lema akisalimia wananchi wa Arusha jana
 ..aliwapa saluti wapiga kura wake kwa uvumilivu
hapa ni wapenda sana wanaarusha.

Alisema akiwa madarakani, hatapenda kuona watu wakiteswa na wanamgambo wa Jiji, hasa wanawake na wafanyabiashara ndogoo na kusisitiza kuwa, hayasemi hayo kwa lengo la uchochezi, bali kama angalizo kwa kuwa siku zote yupo kwa ajili ya kupigania haki na hatarudi nyuma kwa hila yoyote.

Kabla ya kukaribishwa kuzungumza na wananchi, Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema chama chake kimefanya tathimini ya kesi iliyomalizika na kusema wanatarajia kudai fidia ya gharama za kesi hiyo inayofikia  Sh  milioni 253.

Golugwa pia alitumia muda huo kumkabidhi bendera ya Bunge Lema ambayo alikabidhiwa na Mbunge huyo baada ya kuvuliwa nafasi hiyo Aprili mwaka huu.

Alisema alipokabidhiwa bendera hiyo alimwambia aiweke na kusubiri Mungu atende muujiza ambao kwa sasa anasema umetimia kwa Lema kurudishiwa ubunge.

Kuhusu madiwani waliofukuzwa Chadema, alisema kuwa bado anaamini walitendewa haki ya kufukuzwa sababu ya kurubuniwa na huku akiahidi kuwa, uchaguzi ukirudiwa chama chake kitaibuka na ushindi mnono.
Posted by MROKI On Sunday, December 23, 2012 1 comment

1 comment:

  1. Ningeshangaa kama asingetambua hilo maana mji ulipo kweli alipokuwa na kesi ngoja tusubiri maana majani hayatabiriki

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo