Hili si zizi la Mbuzi au banda la
kuku bali ni Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyopo Kijiji cha Kyaseni Kata ya Uru Mashariki, Wilaya
ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro. Ofisi hii
iliyopo katika jimbo la Mbunge Thirili Chami ni miongoni tu mwa ofisi
nyingi za chama hicho katika vijiji vingi nchini ambazo zipo katika hali mbaya huku baadhi ya Vijiji Kama kile cha Kipera,
Kata na Tarafa ya Mlali, Wilayani
Mvomero Mkoani Morogoro vikiwa havina kabisa Majengo ya Ofisi za chama hicho
Tawala jambo ambalo linaathiri utendaji wa Viongozi wa Chama ambao ndio
wameshikilia mhimili wa kuiongoza dola.
December 28, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Fr Kidevu FYI
ReplyDeleteHakuna kata ya Kishumundu. Kishumundu ni KIJIJI kilichopo ndani ya kata ya Uru Mashariki. Kyaseni(sio "Kiaseni") pia ni kijiji ndani ya kata hiyo. Kwa hiyo Kishumundu na Kyaseni pamoja na vijiji vingine 5 (Mnini, Mwasi Kusini, Mwasi Kaskazini, Mruwia, na Materuni) kwa pamoja vinaunda kata hiyo ya Uru Mashariki.
Kwa hiyo:
Ulichoandika hapa ni sawa na kusema Hii ni nchi ya Tanzania iliyopo katika bara la Kenya.
Ni hilo tu kuweka rekodi sawa. Hilo la CCM kufa au kuwa na hali mbaya halina mjadala.
Father Kidevu umeona wenyewe wenye Kishumundu yao wanavyojua Vijiji. Hahahahaa Ila Nape, Mwigulu na wenzenu hebu tuondoleeni hiyo aibu jamani.
ReplyDeleteKazi ya Chama Makao makuu na Vingozi Wakuu wa Chama ni kuwahamsisha vingozi na wanachama wa maeneo yote nchini kujitoa kwa ajili ya kukiimarisha Chama ktk maeneo yao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo ya ofisi za Chama. Kama wana CCM wa eneo hilo wameshindwa kufanya hivyo ni mapungufu ya wana CCM wenyewe wa eneo hilo. Nilazi kuwa wabunifu kama ni kwakuchangishana au harambee ili kuwekeza iwe ktk majengo ya ofisi za Chama au vitega uchumi. Wakiimarika wanachama huko ktk maeneo yao bassi Chama ktk ngazi ya Taifa kitaonekana na kitakuwa imara zaidi
ReplyDelete