Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara,
akimvisha mkanda wa Ubingwa WBF, Francis Miyayusho, baada ya kumtwanga
kwa KO, mpinzani wake Nassib Ramadhan, katika pambano lao la kugombea
ubingwa huo lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba
jijini Dar es Saalaam. Miyayusho alishinda kwa KO katika rauindi ya 10
kati ya 12 za mchezo huo. Kushoto ni mratibu wa oambano hilo,
Bawazir.
Mashabiki wakimnyanyua juu Miyayusho, na kushangilia baada ya kutangazwa mshindi katika pambano hilo.
Miyayusho akishangilia ushindi huo na mashabiki wake huku akiwa na mikanda yote miwili aliyokabidhiwa.
Hapa ni wakati Miyayusho akiingia ukumbini hapo kupanda ulingoni kwa ajili ya kuanza pambano hilo.
Hapa ni wakati Nassib, akiingia ukumbini hapo kupanda ulingoni kwa ajili ya kuanza pambano hilo.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na michezo, Dkt. Fenella Mukangara,
(wa pili kushoto) Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (wa pili kulia) Ben
Kisaka na Mratibu wa pambano hilo, Bawazir, wakiwa meza kuu wakishuhudia
ndonga hizo.
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia pambano hilo.
Mashabiki wa mchezo wa ngumi wakifuatilia ndonga hizo zilizokuwa zikiendelea uliongoni.
Bondia,
Francis Miyayusho (kulia) akimsukumia konde zito mpinzani wake, Nassib
Ramadhan, wakati wa pambano hilo, lililoishia raundi ya 10, kati ya 12
baada ya Nassib kushindwa kuendelea na pambano kwa kuzidiwa.
Miyayusho (kulia) akichapana na Nassib.
Miyayusho (kushoto) akipanga ashambulizi.
Ohooooh!!!
Kushney, ''Nasikia Kizungu zungu kichwa kinaniuma'', Nassib alisikiza
akimwambia msimamizi wake, huku akihesabiwa na mwamuzi wa mchezo huo.
Hapa,
Nassib akijihami kwa kumkumbatia Miyayusho ili kupunguza kasi ya
mashambulizi, jambo ambalo lilimfanya mwamuzi wa mchezo huo kumkata
pointi kutokana na kukumbatia kila mara.Picha zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment