Nafasi Ya Matangazo

December 05, 2012




Kocha wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ameomba ‘fair play’ kutoka kwa muamuzi wa mechi ya leo (kesho) dhidi ya The Cranes ya Uganda katika nusu fainali ya mashindano ya Tusker Cecafa Challenge Cup Jijini Kampala.

Kocha huyo aliyasema hayo mara baada ya Stars, inayodhamniniwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kumaliza mazoezi  katika Uwanja wa Chuo Kikuu Kyambogo.

“Vijana wamejiandaa vizuri kabisa na wote wako katika hali nzuri ya kucheza ila tunachoomba ni fair play kutoka kwa muamuzi maana tunacheza na wenyeji ambao wana watazamaji wengi,” alisema.

Alisema timu zote mbili ni nzuri na iwapo muamuzi atachezesha vizuri basi utakuwa ni mchuano mkali. “Vijana wana ari na mchezo huu na tukipewa fair play tutacheza vizuri kama tulivyofanya katika michezo  dhidi ya Rwanda,” alisema Poulsen.

Muamuzi wa mechi ya Cranes na Stars ni Mohamed El Fadil kutoka Sudan ambaye pia alichezesha mechi ya Stars dhidi ya Rwanda.

Alisema ana furaha kwa kuwa hakuna majeruhi hata mmoja na pia aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha umoja na nidahmmu ya hali ya juu. “Hawa wanakaa kama familia si unawaona walivyo pamoja?” alisema Poulsen na kuongeza kuwa hilo ni muhimu sana kwa mchezaji.

Naye kocha msaidizi, Sylvester Mash alisema Stars ina nafasi kubwa sana ya kushinda mechi hii kwa sababu wenyeji wao, The Cranes watakuwa wanacheza kwa wasiwasi kwa kuwa wako nyumbani .
“Timu yetu iko motivated kabisa na ukizingatia Uganda wako nyumbani, wao ndio wana tension kubwa zaidi,” alisema na kuongeza kuwa mchezo huu utakuwa wa kusisimua sana.

Akizungumza kutoka Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema Stars ina kila sababu ya kutinga fainali na kunyanyua kombe kwa mara ya nne.

“Sisi kama wadhamini tunasubiri ushindi maana tuna imani na Stars na hatua waliyofikia ni nzuri nay a kutia moyo kwa hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi na kuufuatilia mchezo huu kesho,” alisema Kavishe.

Mchezo wa Stars na Cranes utatanguliwa na semi fainali ya kwanza kati ya Zanzibar na Kenya ambao pia ni mchezo wa kusisimua kwani timu zote mbili zimeshaonyesha uwezo mkubwa.

Kocha wa Zanzibar Salum Nassor ameshatangaza mara mbili akiwa Zanzibar na hapa Kampala kuwa iwapo hataondoka na kombe basi atabwaga manyanga.

Fainali na Cecafa Challenge zinatarajiwa kufanyika Jumamosi Disemba 8 na mechi ya kumpata mshindi wa tatu na nne itachezwa siku hiyo hiyo pia.
Posted by MROKI On Wednesday, December 05, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo