Watuhumiwa wa kesi ya Mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira,wakiwa Mahakamani mchana wa leo kabla ya kusomewa hukumu yao.
Askari
wa JWTZ
waliotiwa hatiani hii leo na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa mauaji ya
Swetu
Fundikira, Koplo Ali Ngumbe(Kushoto) na Sajini Rhoda Robert. Watuhumiwa
hawa na mwenzao mmoja Mohamed Rashid wamehukumiwa Kunyongwa hadi kufa.
Hayati Swetu Fundikira enzi za uhai wake.
******
ASKARI wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Sajent Rhoda
Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi waliokuwa
wakikabiliwa na Kesi ya mauaji ya
Marehemu Swetu Fundikira imetolewa leo na Askari hao kuhukumiwa
Kunyongwa hadi kufa.
Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na ndugu jamaa na
marafiki wa Swetu duniani kote ilitolewa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania
jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao watatu wametiwa hatiani baada ya kufanya kosa hilo siku
ya Jumamosi tarehe 23 Januari, 2010 kwa kumpiga bila huruma Swetu Fundikira
katika maeneo ya Kinondoni katika makutano ya barabara za
Mwinjuma na Kawawa jijini Dar es salaam mpaka kusababisha kifo
chake.
Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo vilio vimetawala kwa ndugu
wa watuhumiwa hao huku baadhi ya watu wakidai sheria imechukua mkondo wake
ipaswavyo.
What do we learn out from it?....No one is above the law!.
ReplyDelete