Kulia
katibu Mkuu Ofisi ya makamu wa Rais Bw. Sazi Salula katika ufunguzi wa
warsha ya wadau ya ufuatiliaji na tathmini ya kitaifa wa Kuhimili
mabadiliko ya tabianchi mjini kibaha, leo kushoto ni Mkurugenzi msaidizi
Idara ya mazingira Ofisi ya makamu wa Rais Bw. richard Muyungi.
Washiriki
wa Warsha ya Wadau ya ufuatiliaji na tathmini ya kitaifa ya kuhimili
Mabadiliko ya Tabia nchi, mjini Kibaha.
******
Na Evelyn Mkokoi OMR.
Ufuatiliaji
na tathimini ya kitaifga ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ni njia
mojawapo ya itakayoisaidia Tanzania katika juhudui za apamoja za dunia
za kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula wakati wa ufunguzi wa Warsha ya ufuatiliaji na tathmini ya kitaifa ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
“Wote tumeshuhudia madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, yaliyojitokeza nchini kwetu ikiwa ni pamoja na mvua kubwa zilizonyesha miaka ya hivi karibuni zilizosababisha mafuriko, hali ya ukame, na uhaba wa chakula, alisisitiza.”
Aliongeza kuwa madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi yana athiri nchi na dunia kwa ujumla lakini nchi zilizo maskini zaidi duniani huathirika kwa kiasi kikubwa zaidi.
Bw. Salula alisema kuwa anaamini warsha hiyo itasaidia kupatikamna kwa kablasha ambalo litakuwa na umuhimu kw ataifa hili kwani litasaidia ufuatiliaji na tathmini katika suala zima la kuhimili mabadiliko ya tabaia nchi.
0 comments:
Post a Comment