Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison akiwaonyesha
Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya,na baadhi ya wawakilishi wa wafanya Biashara,
Muswada wa Uboreshaji wa Maswala ya
Usajili wa Meli uliowasilishwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kama sehemu ya
Kuboresha Sheria ya Usajili wa Meli Kisiwani
Humo. Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya wamefanya ziara kwenye Bandari ya Dar
es Salaam ili kuona shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya pamoja na wawakilishi
wa Wafanya biashara wakiwa katika Jengo
la Abiria la Kampuni ya Azam Marine kuangalia namna usalama wa abiria ulivyo
kabla ya kupanda Meli za abiria kulekea Unguja. Mabalozi hao wamefanya Ziara Katika
Bandari ya Dar es Salaam leo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Meneja Uendeshaji wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA), Bw. Patrick Namahuta, akiwapa maelezo ya namna Bandari ya Dar
es Salaam inavyofanya kazi Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya . Mabalozi hao wametembelea
Bandari hiyo leo, kujionea mabadiliko yaliyofanywa na Mamlaka mwaka mmoja baada
ya wao kutembelea Mamlaka hiyo Mwezi Oktoba 2011.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison
Mwakyembe(Mwenye Suti Nyeusi) akipata maelezo ya namna mashine ya kukagulia
Tiketi maalum za Abiria wanaoingia
kwenye Meli kuelekea Unguja kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Kampuni ya Azam
Marine. Waziri wa Uchukuzi aliongozana na Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya na
baadhi ya Wafanyabiashara(Hawapo Pichani), ili kujionea namna ambavyo Bandari
ya Dar es Salaam inavyofanya kazi hasa kwenye swala la Usalama wa abiria .
0 comments:
Post a Comment