Wanafunzi wa mwaka wa pili wa
Chuo Cha St Augustin tawi la Songea wakilaum chuo hicho kwa kutotoa
ushirikiano kwa wanachuo hao kwa sera yao inayosema kuwa hawashughuliki na
mikopo ya wanafunzi.
Kwani sera hiyo imepelekea hadi kutaka kuandamana kwa
wanachuo hao kutokana na chuo kuchelewesha kutoa matokeo yao na kuyapeleka bodi
ya mikopo ikiwa pamoja na majina ili waweze kupata mikopo .
Mmoja wa wanafunzi wa chuoni
hapo amedai hadi sasa bado kuna matokeo amabayo hawaja yapata kutokana na
mkufunzi ambaye ameyazuia kwa sababu hajalipwa mshahara wake. Vilevile
ameshangazwa kwa sela hiyo ya chuo wakati baadhi ya matawi kama Tabora, Bukoba
na Mwanza ambapo ni makao makuu ya Chuo wanaushirikiano na wanafunzo wa vyuo
vyao pia wameshapata mikopo.
Kutokana na hali hiyo
iliwabidi wanafunzi wa mwaka wa pili wachange elfu tano kwa kila mmoja
aliwamkabidhi mmoja wa wahusika wa bodi ya mikopo ambaye pia ni mwanafunzi
akashughulikie mikopo yao lakini bado iliwawia ngumu kutokana na kucheleweshwa
kupelekwa kwa majina na matokeo yao.
Akiendelea kuzungumza mwanafunzi huyo amesma Naye
Profesa Donatus Komba mbaye ni mkuu wa chuo aliondoka na majina pamoja na
matokeo hayo ya wananchuo wa mwaka wa pili na kuyapeleka bodi ya Mikopo wakati
yeye akielekea mwanza katika kikao, lakini pamoja na kupeleka majina na matokeo
hayo kapeleka muda umekwenda cha ajabu hadi sasa mambo bado ni bilabila .SOURCE: DEMASHONES BLOG
0 comments:
Post a Comment