SIKUDHANI
hata kidogo kama Jumatatu ya Novemba 26, 2012 majira ya saa moja niliposimama kwa muda mrefu katika
makutano ya barabara za Mandela na Nyerere zamani Pugu na kuangalia matangazo
kadhaa ya bidhaa za Azam na kuchezwa kwa ufasini mkubwa na Sharo Milionea na
Kig Majuto ndo nilikuwa naangalia maisha ya msanii huyo akiwa ana pumzi.
Baadhi ya
matangazo yalinivutia na kunifanya nicheke hasa lile la Boti ambalo Majuto na
Mkewe walienda kumpokea kijana wao akitoka Zanzibar na alipo tua akaanza
midondo yake huku akijifuta bega na kumfanya Majuto aliyevalia suti nae
kumfatisha.
Dah! Nikiwa mbele ya Komputa yangu nikiendelea na kazi za Kublogua
majira ya saa tatu kasorobo hivi nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu Abdalah
Msuya akitaka kufahamu ukweli juu ya ajali na kifo cha Sharo Milionea.
Mh! Nilistuka nikamwambia sijasikia lolote na ndio kwanza
nimewasha mashine nataka kufanya updates za Blog yangu ya www.mrokim.blogspot au FATHER KIDEVU
BLOG, lakini nikamwambia nipe dakika chache, nikawasiliana na blogger mwenzangu
Ahmad Michuzi nae akaniambia amezisikia ila bado si za uhakika.
Pole
nazituma Faza, mlo wafuasi wa Sharo,
Pole zifike
Muheza, mlio mlea wetu Sharo,
Hili siwezi
libeza, mlaaniwe mlomwibia Sharo,
Pole kwa
tasnia ya filamu, kwa msiba huu wa Sharo.
Uchekapo
huongeza siku, Sharo tunakushuru sote,
Binafsi
uliongeza buku, ukanifanya sebleni nisitoke,
Mama alileta
na kuku, ukatufanya kutwa tucheke,
Pole kwa
tasnia ya mziki, kwa msiba huu wa Sharo.
Niliamua kumpigia simu Kamnada wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP
Costantine Massawe na kuniambia ni kweli kuna ajali imetokea Muheza kijiji cha
Lusanga na kumhusisha msanii Sharo Milionea ila bado hajapata ripoti kamili na
baada ya dakika chache niwasiliane nae.
Nilivuta subira ya dakika tano hadi kumi kasha nika mpigia tena
simu Kamishna Msaidizi huyu wa Polisi na kunipa jibu kuwa Nikweli Sharo
Milionea amefariki katika ajali ya gari majira ya saa mbili usiku.
Hakika ni majonzi kwa kila mtanzania mpenda sanaa ya maigizo,
vichekesho na filamu achilia mbali mziki hapa nchini na ukanda wote wa afrika
mashariki kufuatia kifo cha Hussein ramadhani Mkieti ama Sharo Milionea.
Ni majonzi makubwa sana maana hasa ukiangalia kifo chake kilivyo
tokea kwa msanii huyu, ambaye alikuwa safariki akitokea jijini Dar es Salaam
kwenda nyumbani kwao Lusanga Muheza Tanga kuwasalimu wazazi na akiwa ndio
amekanyaga ardhi ya eneo alilozaliwa la Lusanga akakutwa na umauti kufuatia
ajali ya gari.
Mziwanda
huyu katika familia ya watoto watatu wa Mzee Ramadhani na Zainabu Mkieti,
aliyezaliwa mwaka 1987 katika kijiji cha Lusanga, Muheza, Tanga.
Sharo
Milionea alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Lusanga na baadaye
kujiunga na sekondari ya Kwabutu alikosoma hadi kidato ya tatu alopoacha shule
kutokana na matatizo ya kifamiliaa mabyo huwakumbuka vijana na watoto wengi
duniani kote.
Sharo baada
ya kuacha shule mnamo mwaka 2003 aliamua kuhamishia maisha yake jijini Dar es
Salaam ambako mama yake mzazi alikuwa akiishi na hii ni baada ya kuona mambo kule Lusanga hayasomeki na kuamua kwenda
mjini kupambana.
Akiwa jijini
Dar es Salaam, Sharo alijifunza vitu mbalimbali ambavyo wenyeji wake walidhani
vingemkwamua kimaisha hasa kutokana na elimu ndogo aliyonayo, miongoni mwa vitu
hivyo ni kujifunza umakenika na utengenezaji wa majokofu na ikawa haitoshi na
kufanya biashara ya magazeti maeneo ya Kiwalani.
Mama yake aliamua kurejea Muheza kwenda kumuuguza bibi yake na kujikuta
akiishi peke yake katika jiji hili la Dar es Salaam.
Lakini kuingia
kwake katika sanaa ni katika kuhangaikia tumbo, na mtu aliyemsukuma sana
marehemu Sharo Milionea kuingia katika sanaa ni Siasa Mohamed a.k.a Chiba.
Kundi la
kwanza kuundwa na lilikuwa ni kati ya Sharo, Snura Mushi, Nas na Dats na hii
ilikuwa mwaka 2005 walipo unda kundi hilo la mziki ambalo hata hivyo halikudumu
baada ya mmopja wao Snura kuhamia maigizo na kucheza filamu ya Jumba la
Dhahabu.
Baada ya
kuona mwenzao amecheza filamu hiyo Sharo nae alikacha kundi hilo na kuahamia
katika kundi la Sanaa za maigizo la Jamal Arts lilikuwa chini ya Gumbo Kihorota
na kuonesha makali yake katika filamu ya Zinduna na Itunyama ambayo aliigiza
pamoja na wakali wengine wa vichekesho wanaotamba na kundi la Ze Komedi
Origino, Emmanule Mgaya ‘Masanja, Alex Charamila ‘Macklegan’,.
Historia ya
Marehemu Sharo Milionea ilizidi kupanda na kuanza kujipatia umaarufu na kwa mara
ya kwanza alichukuliwa na Musa Kilali na aliigiza kwenye filamu ya vishekesho
ya Mbwembe vol 2 ambayo aliigiza kama ’Bitoz ’ wa kijijini huko nako aliigiza
na wasanii kadhaa wakiwamo Robert Augustino ‘Kiwewe’ na Christian Masele ‘Masele’.
Baada ya
kufanya vizuri licha ya uchanga wake Msanii mwenzake wa Vichekesho, Kiwewe alifanya
utaratibu na kumuingiza katika filamu ya vichekesho iliyokwenda kwa jina la ‘Vichwa
Vitatu’.
Alifanikiwa
kuigiza filamu hiyo na baade kuigiza filamu zake za Vichekesho za za Sharobalo
na Sharo Milionea.
Miaka ya
hivi karibuni Marehemu aaliingia mkataba mpya kwa kipindi cha mwa mwaka mmoja
na Khalfan Abadallah anayemiliki Kundi la Bongo Super Stars Comedy ambalo
linawashirikisha waigizaji kadhaa akiwamo Kign Majuto na Masele, pia aliigiza
komedi ya Back from New York na Mtoto wa Mama.
Ni hapo
ndipo maneno ya Oh! Mamaa na Kamata Mwizi Meen yalipoanza kuvuma wakati wa
filamu ya mtoto wa mama ikiwa sokoni.
Sharo
Milionea hakika alikua hana tofauti na Mcheza Filamu maarufu diani Will Smith ambaye
anaweza kuigiza komedi, filamu na kuimba.
Binafsi naweza kusema kuwa miongoni mwa wasanii walio weza kuleta
mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu na Ucheshi ni Sharo Milionea maana
awali ilizoeleka kuwa ili mtu achekeshe lazima avae nguo za ajabu lakini kumbe
hata ukivaa smati inawezekana.
Umautio unamfika kijana huyu wakati tayari akiwa amesha shika
chini vizuri na sanaa yake ina mea vilivyo katika anga mbalimbali na kujipatia
tenda na kazi nyingi za matangazo akiwa na nguli King Majuto.
Sharo
Milionea ambaye alionekana na kuzoeleka kuwenye komedi, lakini pia aliweza kuubebea
uhusika wake vizuri katika filamu inayotamba sana ya Chumo iliyoongozwa na
Jordan Riber yenye maudhui ya kupambana na ugonjwa wa malaria.
Akiwa
ameigiza kwa jina la Juma katika filamu hiyo, Sharo Milionea alicheza kama kijana
masikini na ametokea kumpenda Amina (Jokate Mwegello), ingawa baba yake Amina
Ali alitaka binti yake kuwa na maisha mazuri, hivyo kutaka aolewe na Yustus
(Yusuph Mlela) ambaye aliyetoka kwenye familia ya kitajiri.
Mbali na
kucheza filamu Marehemu Sharo Milionea alikuwa na ushirikiano mzuri na wasanii
wengine na hata kushirikiana nao kama alivyo fabya katika wimbo wa ‘Sababu ya
Ulofa” wa msanii Top C.
Kama ilivyo
ada jina la utani mtu hajipi mwenyewe bali hupewa na watu kama si marafiki bali
ni mashabiki wa kazo zako, hata mimi Father Kidevu si kujipa bali nilipachikwa
tu na wa fanyakazi wenzangu pale The Guardian Limited kwa staili yangu ya
ndevu.
Hivyo chanzo
cha jina la Sharobalo, ni mashabiki wake kutokana na staili yake ka kibrazamen
na wale walio kuwa nae watakumbuka kuwa Sharo Milienea tangu akiwa ndogo huko
Tanga suala la usafi lilikuwa jadi yake na hata kama alikuwa na nguo mbili basi
zitazifua, ilimradi aonekane nadhifu.
Aliamua
kubadili jina hilo la utani kutoka Sharobalo hadi Sharo Milionea baada ya
msanii mwenzake Bob Junior kudai ni mali yake na linatumika katika studio yake Sharobalo
Recods hivyo akaamua kujiita Sharo Milionea.
Katika uhai
wake Sharo Milionea muasisi wa Ooh! Mama na kamata Mwizi meen huku ukijifuta
bega na kuvuta mguu mmoja ukiwa umekamatia suruali yako katika flaizi aliwahi
watamka kuwa anawazimikia sana Joti na King Majuto ambaye sasa hadi umauti
unamkuta walikuwa wakifanya kazi pamoja.
Akiwa na
King Majuto pia Sharo Milionea alicheza Filamu ya ‘Alosto’ akiwa na mkongwe
huyo na majuto kuonesha kipaji chake licha ya umri alionao.
Nilisikiliza
mahojiano ya Clouds FM na King Majuto kufuatia kifo cha Sharo Milionea, japo ni
huzini lakini nitaka kucheka pale Majuto aliposema baada ya kupata taarifa za
msiba mwili wake ulifutuka kama pulizo na mishipa ilijaa.
Dah! Kweli
inauma sana dhahiri tulimpenda sana Sharo miliomnea lakini ndop hivyo mauti
yamemfika na kutuacha mashabiki wake wanyonge, kama ilivyo ada tutaendelea kuwa
na imani kuwa tutaonana nao tena wapendwa wetu hawa.
Sharo
Milionea alikuwa na kiu ya siku moja kuigiza na wakali wa vichekesho na vituko
kama Mr Bean, Eddy Murphy na Will thimis, na ni wasanii wa majuu alikuwa
anazimia sana kazi zao na alikuwa haishi kuziangalia.
Sharo
alikuwa na ndoto pia ya kuwa Muigizaji wa kimataifa na mfanya biashara, lakini
zote hizi ndoto zake zimeyeyuka kutoka na kifo kuchukua uhai wake.
Leo hii Father Kidevu Blog hatuna jipya la kusema dhidi yako Sharo Milionea zaidi ya kusema kapumzike kwa amani, na hakika kama kucheka na kufurahi kunaongeza siku za kuishi duniani basi uliongeza sana salio letu la kuishi huku salio lako likikosa muongezaji.
0 comments:
Post a Comment