Nafasi Ya Matangazo

November 28, 2012


Ndege aina ya Airbus A319 ambayo itanza safari zake tarehe 29 Novemba 2012 kwa safari za kutoka Dar es Salaam-Mwanza,Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro. Na kiwango cha chini cha Nauli kitakuwa ni kiasi cha Shilingi za kitanzania 32,000/- kwa tiketi ya Kwenda peke yake.

Baadhi ya Abiria ambao walipata fursa ya kufanya majaribio ya safari ya Ndege ya Airbus A319 ya Shirika la ndege la Fastjet wakiwa ndani ya Ndege hiyo kabla ya Kuruka kuelekea Zanzibar kama sehemu ya Uzinduzi wa Ndege hivyo. Safari za ndege hiyo zitaanza rasmi tarehe 29 Novemba 2012 kwa safari za kutoka Dar es Salaam-Mwanza,Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro. Na kiwango cha chini cha Nauli kitakuwa ni kiasi cha Shilingi za kitanzania 32,000/- kwa tiketi ya Kwenda peke yake.

Baadhi ya abiria wakishuka katika Ndege ya Shirika la Ndege la fastjet  ambalo safari zake zimezinduliwa leo na zitaanza safari zake rasmi tarehe 29 Novemba 2012. Ndege hiyo itafanya safari zake za kutoka Dar es salaam-Mwanza, Dar es Salaam-Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba, akitoa hutuba yake wakati wa Uzinduzi wa Safari za Ndege ya shiirika la Fastjet leo jijini Dar es Salaam. Ndege hiyo aina ya Airbus A319, itaanza safari tarehe 29 Novemba 20120 na  itakuwa ikifanya safari zake kutoka Dar es Salaam-Mwanza,Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba (aliyevaa tai nyekundu), akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya fastJet, Bw. Edward Winter kabla ya uzinduzi wa Ndege ya Shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Bw. Fadhili Manongi.
*******
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha inajipanga kwa ajili ya kuboresha Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro ili kuweza kukabiliana na ongezeko kubwa la abiria watakaokuwa wakitumia Viwanja hivyo, baada ya Safari Za Ndege ya Fastjet kuanza.



Agizo hilo limetolewa leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, wakati akiizundua Ndege ya Shirika la Ndege la Fast Jet jijini Dar es Salaam.



'Nawaagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuhakikisha kuwa wanaviandaa Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro kwa ongezeko la Abiria ambao wanategemewa kutumia Viwanja hivyo. Ni matumani yangu Mamlaka inalichukua swala hili kwa umuhimu wake na itahakikisha kuwa hakuna Abiria atakaeshindwa kusafiri kwa sababu ya msongamano wa Abiria katika Viwanja Vyetu', Alisema Dk Tizeba.



Aidha Dk. Tizeba aliongeza kama sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha Mazingira ya Sekta ya Usafiri wa Anga. Serikali imeweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa Miundombinu ya Viwanja Vya ndege.



"Serikali imeweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa Miundombinu ya Viwanja Vya ndege ambayo inakwenda sambamba mabadiliko ya sheria na maboresho ya kanuni'. alisema Dk. Tizeba.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la fastjet amesema siku ya leo ni siku muhimu sana si kwa Shirika hilo lakini pia na kwa Tanzania na Afrika maana usafiri wa bei rahisi umezunduliwa.



"Leo ni siku muhimu sana kwa Shirika la fastjet, Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa Muda mrefu waafrika hawakuwa na usafiri wa Anga wa Uhakika na wa kuaminika .Fast jet itawawezesha kutumia usafiri wa Ndege na Shirika linatarajia kuwahakikishia usafiri wa bei nafuu kutoka sehemu moja kwenda nyingine'.alisema Bw. Edward.



Edward aliongeza mpaka saa  Shirika limeshaajiri watanzania 70 ambapo miongoni mwao ni  Wahudhumu wa Ndege(Vabin Crews), na watu wa masoko na akaongeza kuwa kampuni itaendelea kuajiri watanzania wengi kadri Shirika litakavyoongeza Ndege zake.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi. Suleiman S. Suleiman amesema Mamlaka imejipanga kwa ajili ya kuboresha Sehemu za kusubiria Ndege na imeahidi kuendana na Mahitaji ya yanayotakiwa.



Shirika la Ndege la fastjet litaanza safari zake Tarehe 29 Novemba 2012 kwa safari mbili kila siku ambazo ni Kuanzia Dar es Salaam-Mwanza na Dar es Salaam-Kilimanjaro.Nauli  ya chini kabisa inakadiriwa kuwa Kiasi cha hilingi za kitanzania 32,000/- na Tiketi ya Juu kabisa inakadiriwa kuwa Shilingi za Kitanzania 92,000/- bei hizo zikiwa bila vat.



Lengo la Shirika hili ni kuvutia abiria wengi zaidi hasa wale wa kipato cha kawaida kuweza kutumia usafiri huo.Na kiwango cha Nauli ni kidogo ili kuwavutia wale ambao hawajawahi kutumia usafiri huo wautumie.
Posted by MROKI On Wednesday, November 28, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo