Mwimbaji chipukizi wa Nyimbo za Injili,
George Haule, amipakua Albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Mwamba ni
Yesu na sasa ipo mtaani.
Akizungumza na Father Kidevu Blog,
mtumishi huyo wa Mungu amesema albam yake ina nyimbo 8 lakini Mwamba ni Yesu
ndio uliyobeba jina la albam yake hiyo ya kwanza.
Haule amewaomba watanzania na wapenzi wa
nyimbo za injili nchini kumuunga mkono katika harakati zake hizo za kumuimbia
Mungu.
Amezitaja nyimbo zilizomo katika labam
yake hiyo kuwa ni Mwamba ni Yesu uliyobena jina la albam, Watakiri Mungu
Mkubwa, Gusa Maisha Yangu, Nimeona Wala sijasimuliwa, Nadunda Mugati Mwa Yesu,
Longa na Yesy, Tunapendeza na Safari na Yesu.
Haule amesema Albam hiyo ni kazi nzuri
iliyofanywa na Waandaaji watatu wa muziki wa Injili, Edwad/Laulence
Nguno na Muba Tach.
Amesema albam
yake hiyo inasambazwa na Kampuni ya Usambazaji ya Umoja Audio Visual EA Limited
au GMC kwa Mamu, na yeyote anaetaka kazi hiyo afike kwa wasambazaji hao.
Haule anatoa
shukrani zake za wachungaji,
viongozi na wa umini wote wa BCIC, Temeke kwa maombi yao pamoja na wote walio
pokea ujumbe wa albam yake na wakabarikiwa
na wakaniombea.
Haule namalizia kwa kusema “Mungu hawezi
kumuacha Mwanadamu anae mtii amina.”
Kwa Mawasiliano zaidi ni
+255 752644040 au +255 802405
Barua pepe: ghaule@rocketmail.com
0 comments:
Post a Comment