Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kushoto) akiongea na
waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari ya
Umma unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Serikali
imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba
za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma . Baada ya
hapo Operesheni hiyo iitakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya
umma,Vilevile kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST,
PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya
moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma. Pamoja nae ni kamansda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi, James Mpinga. (Picha
na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment