Nafasi Ya Matangazo

October 06, 2012

JUMLA  ya warembo 29 kati ya 30 wanaowania taji la REDDS MISS TANZANIA 2012 leo wameanza ziara rasmi ya kutembelea Vivutio vya Utalii vilivyopo Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Moshi, Arusha na Manyara.

Warembo hao wakiongozwa na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, wakiwa katika mikoa hiyo watatembelea vivutio hivyo na kuhamasisha jamii ya watanzania kuwa na desturi ya kutembelea vivutio hivyo vyua ndani na kuhamasisha utalii. 

Pia warembo hao watapata fursa ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na masuala ya utalii. Oktoba 7, warembo hao watatembrelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, katika lango kuu la kupandia Mlima huo la Marangu. 

Aidha kwa mujibu wa ratiba hiyo, inaonesha kuwa warembo hao watafanya tamasha la Michezo mjini Arusha kabla ya kuelekea Monduli ambako Oktoba 8 watazuru Kaburi la Waziri Mkuu wa Zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine.
 Mrembo Fatma Ramadhani kutoka Kanda ya Elimu ya Juu akiangalia vijana wafanya biashara wadogo wa bidhaa za mkononi kituo cha Chalinze.
 
 Misosi ni muhimu bwana kwa warembo, hapa wakiwa Korogwe High Way wakipata kitu ile roho inapenda.
 Hawa waliamua kushow love kabla ya kupata mlo wao.
 Washiriki hawa wa Redds Miss Tanzania 2012 wao walisema waweke Nakadhalika katika Menu yaoo hapo sasa wana fanya mambo.
 Mary Chizi aliamua kushow love na wahudumu wa jiko la msosi hapo High Way, yes mrembo lazima ujichanganye na uwe mtu wa watu.
 Kila mmoja wao alikamatia chakula hakuna asiyekula labda ambaye amefunga.
 Safari iliendelea kwa gari lililobeba warembo kushika barabara 
 Stori zikaendelea huku safari ya kuitafuta Moshi mkoani Kilimanjaro ikinoga.
 Kunywa na kutafuna havikukoma na warembo wa Redds Miss Tanzania walijinafasi.
 
 Tabasamu kwa mpigapi na Camera jamani
 
 Wahenga walinena "shibe mwana Malevya Njaa Mwana Malegeza" haya sasa Shibe ikaleta Usingizi na hawa waliamua kulala kidogo kupunguza uchovu wsafari.
Safari iliendelea hadi tukafika Moshi ndani ya Snow View Hotel Wilayani Hai.
Posted by MROKI On Saturday, October 06, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo