Michezo ya Bandari maarufu
kama ‘inter-ports games’ imeanza rasmi katika viwanja vya CCM Kirumba jijini
Mwanza ambapo mashabiki wameonesha kuridhishwa na michezo ya awali ya ufunguzi
huku wachezaji wakionesha vipaji vya hali yajuu katika michezo ya soka, mpira
wa kikapu, pete na kuvuta kamba.
Michezo hiyo ambayo imefunguliwa
na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (MB),aliyefurahishwa na kuridhishwa
na maandalizi yake, inategemewa kufanyika kwa muda wa siku tano kuanzia Agosti
15 katika jiji la Mwanza.
Dk. Tizeba amewaasa wachezaji
kucheza kwa upendo na staha na kukumbuka kwamba michezo inajenga undugu na
mshikamano na si uadui. Aidha amewakumbusha wachezaji kuendelea kushiriki katika
michezo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha afya zao mara baada ya kukamilka kwa
michezo hii.
Michezo ya ‘inter-ports games’
inazikutanisha bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Mwanza, Kyela, Kigoma
na Makao Makuu ambapo michezo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba, bao, riadha,
kikapu na mprira wa pete itashindaniwa.
Mchezo wa Bao nao upo na hapa wakichuana
Wanaume
wa shoka wa mchezo wa kuvuta kamba kutoka Dar es Salaam port wakiwania ushindi.
Mashabiki wakifuatilia michezo hiyo ndi ya uwanja wa Kirumba jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment